Kutoa damu yote kwa wakati mmoja huyo mtu akaendelea kuishi, haiwezekani.
Humu mwilini damu haikai labda kwenye kipipa kiasi iwe shughuli ya kuimwaga tu, kuna vimishipa uzi mnene, vimesambaa kama utando wa buibui, shughuli ya kutoa damu huko kote ikaisha kwa wakati mmoja halafu iishe kabisa labda kwenye teknolojia ijayo.
Virusi vinakaa kwenye seli za damu ambazo zinaweza kupenya nje ya mishipa ya damu, sasa hivyo tukitoa damu yote tutakuwa tumeviacha.
Bado wanadamu hawajaweza kutengeneza damu maabara. Mwanadamu kwa kawaida asipokuwa na upungufu, anakuwa na damu lita tano zinazunguka. Kupata drip moja ya damu ambayo hata lita moja haifiki mpaka leo ni changamoto na watu wanakufa kwa kukosa hiyo dripu moja tu. Hizo lita zitatoka wapi.
Nimejaribu kukuelewesha kitoto, wakati mwingine hata ukiwaza tafakari hoja yako mwenyewe halafu ifikirie kama ingekuwa rahisi kwa nini mpaka leo kuna watu kutwa kazi yao ni kujaribu kama wanaweza hata kutoa kinga.