Tiba ya UKIMWI

Tiba ya UKIMWI

Sodium

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2014
Posts
754
Reaction score
404
Nimekuwa nikifikilia jinsi ya kupata tiba ya ukimwi na nikakuta kuwa ukimwi unapatika mwilini mwabinadamu na hasa hasa kwenye damu, nikafikili kama mtu mwenye UKIMWI ataondolewa damu yote yenye virus vya ukimwi na kuwekewa damu salama hawezi pona ? nakaribisha mawazo yenu wakuu
 
Nilikuwa najiuliza kwanini somo la biolojia o-level ni la lazima (compulsory) leo ndio nimepata jibu! Hivi mkuu uliyeleta mada ulishawahi kuona sehemu ya ndani ya mifupa ya ng'ombe hapo buchani? Huo wekundu katikati ya mifupa ndio hapa sehemu ya damu inatengenezwa, na hapu utapachokonoa 'ku-flash' virusi ukimwi? Na ujue virusi sio kama chawa ati....elimu haina mwisho jaribu kujisomea hata 'wikipidia' mkuu huo uzushi wa flani huwa anaenda sauzi kumwaga damu yake yenye ukimwi kama 'oil chafu' waachie wenyewe!
 
Nimekuwa nikifikilia jinsi ya kupata tiba ya ukimwi na nikakuta kuwa ukimwi unapatika mwilini mwabinadamu na hasa hasa kwenye damu, nikafikili kama mtu mwenye UKIMWI ataondolewa damu yote yenye virus vya ukimwi na kuwekewa damu salama hawezi pona ? nakaribisha mawazo yenu wakuu

Muda si mrefu litaanzishwa daraja jingine la matokeo ya form four, DIVISION SIX!
 
Ndebile inabidi umsaidie tu maana ndo kashauliza. Sodium icho kitu hakiwezekani, unajina lakisayans ila umeuliza swali dogo sana la sayans
 
Last edited by a moderator:
Haya ndiyo matokeo tunayojivunia ya Big Results Now kwenye sekta ya elimu!
 
Nimekuwa nikifikilia jinsi ya kupata tiba ya ukimwi na nikakuta kuwa ukimwi unapatika mwilini mwabinadamu na hasa hasa kwenye damu, nikafikili kama mtu mwenye UKIMWI ataondolewa damu yote yenye virus vya ukimwi na kuwekewa damu salama hawezi pona ? nakaribisha mawazo yenu wakuu
Mkuu ningependa kujua una umri gani?
 
Aisee mi nilijua dawa ishapatikana...Lol
 
Kauliza swali dogo sana la sayansi badala ya kumjibu mnamshambulia,nyie mliosoma biolojia mpeni jibu!
 
Kutoa damu yote kwa wakati mmoja huyo mtu akaendelea kuishi, haiwezekani.

Humu mwilini damu haikai labda kwenye kipipa kiasi iwe shughuli ya kuimwaga tu, kuna vimishipa uzi mnene, vimesambaa kama utando wa buibui, shughuli ya kutoa damu huko kote ikaisha kwa wakati mmoja halafu iishe kabisa labda kwenye teknolojia ijayo.

Virusi vinakaa kwenye seli za damu ambazo zinaweza kupenya nje ya mishipa ya damu, sasa hivyo tukitoa damu yote tutakuwa tumeviacha.

Bado wanadamu hawajaweza kutengeneza damu maabara. Mwanadamu kwa kawaida asipokuwa na upungufu, anakuwa na damu lita tano zinazunguka. Kupata drip moja ya damu ambayo hata lita moja haifiki mpaka leo ni changamoto na watu wanakufa kwa kukosa hiyo dripu moja tu. Hizo lita zitatoka wapi.

Nimejaribu kukuelewesha kitoto, wakati mwingine hata ukiwaza tafakari hoja yako mwenyewe halafu ifikirie kama ingekuwa rahisi kwa nini mpaka leo kuna watu kutwa kazi yao ni kujaribu kama wanaweza hata kutoa kinga.
 
Double R nimekuelewa ila watu wanaogundua mambo kama hayo ni watu kama sisi so tusichoke kufikiria tiba ya ili gonjwa
 
Umri wa nin wewe toa mawazo
 
Back
Top Bottom