Tetesi: TIC imedorora, wawekezaji wayeyuka!

Mwenye alihudhuria Yale maonyesho ya TIC ya Mwanza pale Rock city mall atuambie hali ilikuaje
 
Hata kipindi kile mlidai VAT Katika Utalii itafukuza wataliii, dua Yenu haikupokelewa
 
Mkuu unaota wewe, hayo maneno unamezeshwa na wazalendo uchwara ambao hawajawahi kufanya biashara yoyote na hawana lolote wajualo kuhusu biashara. Kwa sera hizi nchi hii inaenda kuwa fukara moja kwa moja. Hizi hadithi za nchi kuwa nchi bora alikuwa nazo Nyerere, akataifisha mali za matajiri. Kilichokuja kutokea ni wananchi kuvaa viraka na hadi anatoka madarakani nchi ilikuwa imekuwa masikini wa kutupwa.
Je ulikuwa unaridhika na upigaji uliokuwepo TZ?. Hata kama tulikuwa tunanufaika na uzembe ule wa Serikali lakini haukuwa endelevu.
Sasa hivi tunapitia kipindi cha mpito kabla ya kuanza kunufaika, lakini kwa wale tu wanaochapa kazi.
 
Tunaelekea nchi ya viwanda .zee comedy.tutapata tabu sana
 
Unapelekwa mahakamani Tanzania jaji au hakimu hajui hata matumizi ya teknolojia kichwa chake kiko rigid hana exposure hahahaha
 
Kuna tetesi kuwa idadi ya wawekezaji wapya kupitia kituo cha Uwekezaji, TIC imepungua sana ndani ya miaka miwili iliyopita.

Waekezaji wengi, inaelezwa, wanachungulia hali na kuahidi kurudi, lakini wanaishia.

Tujitahidi Watanzania tuwekeze wenyewe.
Acha umbea mtoto wa kiume, unapotosha watu bila ya kuwa na takwimu??,hujui kusema hivyo bila ya kuwa na takwimu ni kosa??

Wewe ndio msemaji wa TIC? Nani kakupa mamlaka ya kuisemea serikali?

Unaongea with zero statistics ambazo si sawa na za TIC hujui kwamba unavunja sharia ya takwimu ya mwaka 2015??

Ni kwanini usichukuliwe hatua za kisheria?
 
Duh mkuu hilo deni si bei ya bombadia
Nchi ya ajabu kweli tra walikuwa kila mwaka wanakukadiria kodi unayotakiwa kuilipa na unailipa baada ya kujirizisha kuwa ndio unastahili kulipa!!baada ya miaka mitano wanakuja na kukwambia kuwa kumbe walikosea makadirio ya kodi ,wali kadiria kidogo hivyo kila mwaka kuna tofauti ya milioni kama 300!!hivyo una deni la 1.5 bilioni!!!haaaaa wakati hiyo pesa hata kuitia mkononi hujawahi,ndio kinachowakuta wau sasa!!!!ndio wanakuja mala ohooo tukae chini tujadiriane jinsi ya kuyafuta!!!kuna jamaa mmoja alikuwa muuza vinywaji vya jumla anadaiwa zaidi ya bilioni 300!!!
 
Acha umbea mtoto wa kiume, unapotosha watu bila ya kuwa na takwimu??,hujui kusema hivyo bila ya kuwa na takwimu ni kosa??

Wewe ndio msemaji wa TIC? Nani kakupa mamlaka ya kuisemea serikali?

Unaongea with zero statistics ambazo si sawa na za TIC hujui kwamba unavunja sharia ya takwimu ya mwaka 2015??

Ni kwanini usichukuliwe hatua za kisheria?
Ninkosa la jinai kutoa statistics!
Upo hapo?
 
Acha umbea mtoto wa kiume, unapotosha watu bila ya kuwa na takwimu??,hujui kusema hivyo bila ya kuwa na takwimu ni kosa??

Wewe ndio msemaji wa TIC? Nani kakupa mamlaka ya kuisemea serikali?

Unaongea with zero statistics ambazo si sawa na za TIC hujui kwamba unavunja sharia ya takwimu ya mwaka 2015??

Ni kwanini usichukuliwe hatua za kisheria?
Mwita muraa!
Uwekezaji siyo amri ya jeshi, kama kwenu mlivyozoea.
Sheria lazima ziwe karibishi kwa mitaji toka nje.

Sheria ambazo kimsingi ni prohibitive hazisaidii uwekezaji.

Kwa taarifa yako ukikariri hizo sheria za takwinu, hazikusaidii sana kwa sasa maana mitaani tunaona uhalisia yanayo tokea.
 
Huu ni msimamo hasi kwa uwekezaji.
Viongozi si wawekezaji, wao wako upande wa matumizi tu ya kodi, hawazalishi.

Sasa juzi sheria ya Arbitration imepitishwa Bungeni.
Ati mkikosana na muwekezaji itakuwa marufuku kwenda kukubaliana nje ya nchi(Arbitration), kwa taratibu za kimataifa.

Nategemea hili ndo litawakimbiza kabisa hata wale wachache waliokuwa na mawazo ya kuja Tanzania.
Time will tell.
Wa kulaumiwa nini.Tunasaini mikataba bila ya kusoma na kwa kificho.
 
Hili ndilo tatizo la uwekezaji nchini, angalau wawekezaji wa kigeni na mitaji yao huko waliyopewa na serikali zao au mabenki yao, akifika nchini anapewa muda wa kujiimarisha (Tax holiday kwa mambo mengine).

Sasa turudi kwa wazawa, kwa waliojiajiri katika sekta mbalimbali mtakubaliana nami na kama kuna kaeneo mtanisahihisha pia. Nachukulia umeamua kufungua duka au Ka Min-Super Market mtaani kwako.

Mahitaji ili uanzishe:
  1. Mtaji wako- hii mara nyingi utajijua mwenyewe utakapo pata, ukienda kwenye taasisi za mikopo wanakuambia hatukopeshi kuanzisha baki iliyosimama na ulete bank statement kuonesha mzunguko wa hela yako (MFANO UMEKOMAA UKAWA NA MTAJI hela ghafi ya Tsh. 1,000,000/-)
  2. TIN hii haina usumbufu kwani utaipata bure, na hii inamaanisha umeamua kuwa mzalendo uje kulipa kodi
  3. Leseni ya Biashara-Either kutoka halmashauri au manispaa au jiji kulingana na eneo ulipo. Hapa ndio shida inaanza maana unatakiwa kulipia leseni ya Mwaka mzima (mwaka wa kiserikali mfano July,1st 2017-June 30th 2018 Jumla 70,000/-), na hapa utatoa tuu maana haijalishi umeanza April 2018 au May 2018. Na ili uipate hiyo unatakiwa kwenda TRA upate TAX CLEARANCE. Na pia ile form kujaziwa na kuwekwa mihuri, Mtendaji Mtaa/kijiji na Kata, Afisa Afya na huku kote huwezi kutoka hivi maana utaambiwa hela ya muhuri tufanye kotee ni 30,000/-
  4. TAX CLEARANCE-Ukirudi hapa wanakukadiria kodi ya shughuli/biashara yako kwa kuangalia kalenda ya mwaka na wameziweka kwa robo kwaka (Jan-March,April-JUne, July-Sept na Oct-Dec) na hii watakucharge kwa mwaka husika bila kuangalia umeanza lini, mfano umeanzisha biashara November na ukakadiriwa mfano 320,000/- itakubidi uitoe ili upate clearence ndo uendelee na leseni, sawa kunaoption ya kupunguza kiasi, ila mwisho wa siku hiyo hela utaja ilipia japo ulikuwa hujaanza biashara.
  5. Mfano Duka hilo lina vinywaji hasa pombe take away then utatakiwa kwenda Kupata leseni ya hivyo vinywaji napo utakadiriwa na hiyo hela unaitoa in advance mfano hata iwe 50,000
  6. Maadamu ni duka maanake lina vyakula utatakiwa kwenda TFDA ili upate leseni yao napo inahitajika hela in advance mfano hata 100,000
  7. Mwisho eneo umekodi na kodi kwa mwezi mfano 20,000 na mara nyingi unatakiwa kulipa mwaka au miezi sita (240,000 au 120,000/-)
Huuu ni mfano tuu wa mtu wa kuanza kujikwamua awekeze na kujiajiri Je, Jumla ya hela inayotakiwa itolewe kabala hajajua biashara yake itaendaje na je itafaa au la?
KODI NA GHARAMA ZINGINE IN ADVANCE:70,000+30,000+320,000+50,000+100,000 + 240,000 = 760,000
MTAJI UTAKAO BAKIA KUNUNUA VITU = 1,000,000 - 760,000 = 240,000

Hebu ona HUYU MZALENDO kaamua kufuata sheria na taratibu zote zilizowekwa ili asisumbuliwe anabakiwa na hela ya kuanzia 240,000 kutoka Milioni moja aliyokuwa nayo. Je, kwa namna hii serikali haioni kuwa inawashawishi watu wakwepe au kupita njia sisizo sawa ili ajitengenezee kamtaji ili akija kulipia angalau awe kapiga kahatua? Ambapo risk yake akikamatwa kabla atajikuta kafilisika gafla?

Nini Ushauri wangu kwa uwekezaji wowote nchini:
Mtu yeyote anayetaka kuanzisha biashara au uwekezaji kuwe na kipindi maalumu cha kuona uwezekano wa biashara yake kujiendesha. Afuate taratibu zote kupata vibali ambapo apewe bure na baada ya miezi 3 atembelewe kuona shughuli yake na kukadiriwa kodi husika, itawainua vijana. Na isiwe biashara zote ziwe kwa miezi 3, bali zitengwe kwa magroup na kutathmin muda maalumu wa kupewa kujiimarisha kabla ya kuanza kulipishwa kodi. Na atakaye kiuka hayo masharti adhabu na penalt ni halali yake. Na hata kodi pia za kutozwa zisiwe za kukomoa. Hii itafanya wote wawe wazalendo na watalipa kodi bila shuruti.

Kwa wawekezaji wakubwa pia waangaliwe nao namna ya kutengeneza sera shirikishi na si hizi za kutishiana itafanya watu waogope maana hana uhakika wa kurudisha alichowekeza kwenye nchi inayobadili sera zake muda wowote na kwa matamko tuu.

Walipe kodi, kabla ya kuja!
 
Asante mkuu kwa kudadavua mahitaji ya kulipa kodi, tozo na vibali kabla ya kuanza biashara kwa mtu mzalendo.

Kwa mentality iliyopo ni kwamba UKITAKA KUFANYA BIASHARA basi wewe ukubali kuwa MTUMWA WA KODI.

Yaani kabla ya hata biashara yako kuanza, lipia kodi hilo wazo tu!

Tuna mawazo ya kimasikini kwa msimamo huo.
 
  • Thanks
Reactions: ELX
Back
Top Bottom