Tuandamane
JF-Expert Member
- Feb 2, 2008
- 1,221
- 55
""mkuu Single D"
Uko Right Kabisa Hawa Watu Wanatuibia Kwa Kubadili Majina Ya Kampuni Huku Mmliki Yuleyule .....just For Breaking News Waheshimiwa Wa Celtel Wanabadilisha Jina Kuanzia July Wataitwa ""zein"" Kukimbia Kodi Hii Ndio Tanzania Tajirisha Kichwa Chako Utajiri Tosha Naona Watanzania Wanazidi Kuumia ,,,haya Tujipe Moyo......
...
My take:Karamagi ang'olewa uenyekiti TICTS
Na Gladness Mboma
BODI ya Kampuni ya Kupakia na Kupakua Makontena Bandari ya Dar es Salaam (TICTS) imemng'oa madarakani aliyekuwa Mwenyekiti wake, Bw. Nazir Karamagi.
Bw. Karamagi ambaye pia ni Mbunge wa Bukoba Vijijini (CCM), amefikwa na tukio hilo ndani ya kipindi cha miezi mitatu tangu alipojiuzulu wadhifa wake wa Waziri wa Nishati na Madini, kutokana na kashfa ya mkataba wa zabuni ya kufua umeme kati Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) na Kampuni ya Richmond.
Kutokana na mabadiliko hayo, Bodi hiyo sasa itaongozwa na Mkurugenzi wa Kundi la Hutchison Port (HPH) ambalo ni kampuni mama ya TICTS, Bw. John Maredith.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mwakilishi wa Kampuni ya HPH kutoka Hong Kong, China, Bw. Neville Bissett, alisema uamuzi huo umetokana na mkutano uliofanyika Mei 8 mwaka huu.
Bw. Bissett alipoulizwa na waandishi wa habari kuhusu hatma ya hisa za Bw. Karamagi na hatua ya kuondolewa kwake kama inahusiana na tuhuma za ufisadi zinazomkabili, alisema hisa za Mwenyekiti huyo wa zamani ziko pale pale na kubainisha kwamba kuondolewa kwake hakuhusiani na tuhuma hizo.
Akizungumzia utendaji wa TICTS, Bw. Bissett, alisema anatiwa moyo na mafanikio makubwa yaliyopatikana chini ya menejimenti ya kampuni hiyo.
"Ujazo wa makontena ulikuwa wastani wa uniti 20 mwaka 2000 wakati mkataba unaanza, hadi mwaka jana ulifikia uniti 344,000. TICTS imefanikiwa kukuza biashara katika bandari ya Dar es Salaam, hivi sasa ukuaji huo umefikia asilimia 16 ikilinganishwa na asilimia nne tu kabla ya kuanza shughuli zake bandarini hapo," alisema Bw. Bissett.
Alisema mafanikio hayo yamepatikana mbali ya matatizo ya ufinyu wa nafasi unaoikabili bandari hiyo. Alisema tayari TICTS imewekeza dola milioni 21 za Marekani tangu kuanza kwa mkataba huo, kiasi ambacho kinakwenda mbali sana kikilinganishwa na mipango ya awali ya uwekezaji wakati ule wa ubinafsishaji ilivyokuwa.
Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo, Bw. David Cotty, alisema tangu kuongezwa muda wa mkataba mwishoni mwa mwaka 2005, TICTS imejitahidi kukabiliana na uhaba wa nafasi bandarini hapo kwa kubomoa maghala yaliyokuwa hayafanyi kazi ili kupata nafasi zaidi.
Alisema wameingiza vifaa muhimu kwa kazi za upakuaji na upakiaji makontena na yote yamefanyika kutokana na kuongezwa muda wa mkataba
Bw. Cotty, alisema kiasi cha zaidi ya dola milioni 60 za Marekani kitawekezwa kwenye vifaa na upanuzi wa miundombinu katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
Akizungumzia uendeshaji shughuli za bandari katika mazingira ya ufinyu na nafasi, alisema kwa mwaka jana, alisema licha ya kampuni hiyo kuwa na haki pekee kushughulikia meli zenye makontena, waliiruhusu Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kushughulikia meli zenye makontena kwa kuangalia matakwa ya wakati na idadi.
"Kwa sababu nafasi ilikuwa finyu kwa TICTS, lengo likiwa kupunguza msongamano...suala hili la nafasi linabaki kuwa gumu, msimu wa wingi wa makontena ukikaribia, kuna haja ya TICTS kupatiwa nafasi zaidi kwa ajili ya kuhifadhi makontena, pia hatua za haraka zinapaswa kuchukuliwa ili kuepuka makontena kuachwa bandarini zaidi ya muda wa mwisho uliowekwa," alisema Bw. Cotty.
Mwenyekiti mpya wa Bodi hiyo, Bw. Meredith alisema ameridhishwa na jinsi Serikali ilivyounga mkono kuongezwa mkataba wa TICTS na kwamba ni muhimu kwa maendeleo ya muda mrefu wa bandari hiyo.
Alisema TICTS imedhamiria kuendelea kujikita katika maendeleo ya kitengo cha makontena na kwamba jitihada zinalenga kuifanya Tanzania iwe na bandari yenye ufanisi zaidi katika Afrika Mashariki.
Bw. Meredith aliwataka wadau wote kufanya kazi kwa ufanisi na kuchukua hatua, ili kupata suluhu inayofaa katika kuwezesha ufanisi wa operesheni za bandari.
Juhudi za kumpata Bw. Karamagi kuzungumzia hatua hiyo hazikuzaa matunda kutokana na simu yake kuzimwa muda wote gazeti hili lilipomtafuta jana.
Source: Majira

Hapa ni ujanja ujanja tu kumbe TICTS na wachina wamo du hii sasa balaa yaani wazee wa feki wamo....dah tumeliwa.Hapa dawa ni kuvunja mkataba tu jamaa waondoke tu.Wanataka kuwekeza hizo $60mil. toka hapo mwanzo walikuwa wapi??Kwa hiyo wameona mambo magumu ndo wanataka waanze kutupooza kishikaji hapo tusipo komaa hawa jamaa wataendelea kuwepo.
My take:
1. Hawa jamaa (TICTS na Karamagi) wameona Mtanzania ukimuwekea 'issue ya management' ya Wazungu tunakuwa mandondocha (NetGroup, Citywater, etc.)
2. Mwenyekiti mpya anasifia $erikali kuongeza muda wa mkataba na TICTS; Je, maadhimio ya Bunge hayatatekelezwa tena? Au anajaribu kushawishi muda ulioongezwa usipigwe pangwa?
3. Wana mpango wa kuwekeza dola millioni 60 ndani ya miaka mitano ijayo (janja ya nyani)! Kwani walikuwa wapi tangu wapate tenda takribani miaka nane iliyopita?
4. Ninanusa harufu ya mchezo mchafu na inabidi tuwe madhubuti. Wanafanya hivi tuogope, wakidhani tuko dhaifu kwenye masuala ya sheria hasa pale watapotishia kwenda mahakamani tutapokiuka amri ya Mkapa na Mramba.
4. Swali, wana nia njema hawa?? Walikuwa wapi kuboresha (au kutoa taarifa ya uboreshaji) mpaka baada ya wananchi kupiga kelele?
Mie siko tayari kufungwa bao la kisigino tena na nitakuwa tayari kusema nachokijua kabla hawajashtuka
Gembe, Single D, ...mi nasubiri kuyaona ya FILAUNI; hakika hapa ndipo watapoona nguvu ya UMMA!single D said:Ina maana lile bunge pamoja na kamati yake havina maana ktk yale waliyoshauri serikali? Pamoja na kutumia kodi za wananchi kutembelea bandarini na kupeleka maoni kwenye mjengo kule Dodoma bado ushauri unapigwa teke.Nini maana ya bunge la viwango na kasi? Udhalilishaji wa maoni ya wote wanoingia mjengoni mle. Au hizi ndo siri za mambo ya sirini ya baraza la Mawaziri zisemwazo kwenye viapo