Ukipitia mjadala huu wote na wachangiaji wake tangu 2008 basi utagundua ni kwa kiasi gani nchi yetu TANZANIA ilimuhitaji sana Rais mwenye kariba ya MAGUFULI. Bahati mbaya awamu zilizopita ziliponzwa sana na mtandao/makundi yaliyowaingiza madarakani pamoja viongozi hao kukosa uthubutu na zalendo wa dhati katika mioyo yao. Mungu kasikia kilio chetu, leo tumempata JPM mwenye uthubutu, asiye na chembe ya uoga, mwenye uzalendo ndani ya moyo wake. RAIS JPM wengi tunakuelewa kwa kazi ngumu unayoifanya, wachache wasiokuelewa leo watakuelewa kesho!!!