Tido Mhando: Azam TV itarushwa mechi za ligi kuu

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
Uongozi wa Azam Media kupitia Mkurugenzi wake, Tido Mhando, umeibuka na kukanusha taarifa zilizoelezwa na Rutunga M kuwa hawatoonesha mechi za Ligi Kuu Bara msimu ujao.

Mhando amefunguka na kueleza kuwa taarifa zilizosambaa katika mitandao mbalimbali zikieleza kuwa Azam haitorusha mbashara mechi za ligi msimu wa 2018/19 si za kweli.

Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa Azam bado wana misimu mitatu hivyo mkataba wao utakapomalizika watakuwa tayari kufanya mazungumzo mengine ya kuongeza lakini si kweli kuhusiana na yaliyoripotiwa jana.

Ikumbukwe Azam Media waliingia mkataba na TFF kupitia klabu zote za ligi na kusaini mkataba wa kurusha mechi za ligi mpaka msimu wa 2020/21 ambapo mkataba huo utakuwa unamalizika.

"Si kweli kwamba tutasitisha kuonesha, hizo habari hazina ukweli wowote, tutaendelea kama kawaida na mkataba wetu unaoenesha bado tuna misimu mitatu ya kuendelea kuonesha mechi hizo" alisema.
 
Safi sana TIDO, Safi sana Azam. BTW Mr. Tido, vp ile kesi kule Kisutu?
 
bora wasionyeshe maana vifurushi vyao ghali sana, serikali iwapokonye kibali iwape startimes maana ina mkono wake na vifurushi vyake ni nafuu sana
 
startimes wakuda sana nilikua nalipia kifurushi cha 18k kwa ajili ya channel ya SPARKS only sababu ndio my fav channel, cha ajabu wameitoa channel kimyakimya.... ilinibidi niweke king'amuzi store shenz type
 
basi wawape dstv maana ndicho king'amuzi bora
 
Tutegemee bei ya vifurush vyao kupanda
 
startimes wakuda sana nilikua nalipia kifurushi cha 18k kwa ajili ya channel ya SPARKS only sababu ndio my fav channel, cha ajabu wameitoa channel kimyakimya.... ilinibidi niweke king'amuzi store shenz type
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] aiseee Pole mkuu
 
Uongozi wa Azam Media kupitia Mkurugenzi wake, Tido Mhando, umeibuka na kukanusha taarifa zilizoelezwa na Rutunga M kuwa hawatoonesha mechi za Ligi Kuu Bara msimu ujao.

Mhando amefunguka na kueleza kuwa taarifa zilizosambaa katika mitandao mbalimbali zikieleza kuwa Azam haitorusha mbashara mechi za ligi msimu wa 2018/19 si za kweli.

Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa Azam bado wana misimu mitatu hivyo mkataba wao utakapomalizika watakuwa tayari kufanya mazungumzo mengine ya kuongeza lakini si kweli kuhusiana na yaliyoripotiwa jana.

Ikumbukwe Azam Media waliingia mkataba na TFF kupitia klabu zote za ligi na kusaini mkataba wa kurusha mechi za ligi mpaka msimu wa 2020/21 ambapo mkataba huo utakuwa unamalizika.

"Si kweli kwamba tutasitisha kuonesha, hizo habari hazina ukweli wowote, tutaendelea kama kawaida na mkataba wetu unaoenesha bado tuna misimu mitatu ya kuendelea kuonesha mechi hizo" alisema.
Simuamini huyo mzee , mpaka leo ameshindwa kusema kwanini Azam two wameondoa Taarifa ya habari
 
startimes wakuda sana nilikua nalipia kifurushi cha 18k kwa ajili ya channel ya SPARKS only sababu ndio my fav channel, cha ajabu wameitoa channel kimyakimya.... ilinibidi niweke king'amuzi store shenz type
azam nayo imeanza kufeli
 
Back
Top Bottom