Tigo Acheni Wizi, Mnakata Shs45 kila siku Unreasonably

ExpertBroker

JF-Expert Member
Joined
Jun 1, 2009
Posts
454
Reaction score
107
NIMEPOST HII KWENYE PAGE YA TIGO WAMEIFUTA IN A SECOND!!!......... "Nawasiliana na Mwanasheria wangu kwa wizi unaofanywa na TIGO! Nimefuatilia kwa wiki moja sasa baada ya kupuuzia muda mrefu nilichokuwa naambiwa! Nimekuwa naangalia salio kabla sijalala, lakini kila ikifika saa6 usiku, TIGO wame-set ikatwe shs 45 kila siku! Kama wewe ni mteja wa TIGO, fuatilia hili!! Japo yaonekana ndogo, lakini Shs45 kwa siku, kwa watu million mbili kwa mfano, ni sawa na Shs90 Million kwa siku, sawa na Shs 2.7 billion kwa mwezi, pesa ya mishahara ya staff wenu na masalia kibao! WIZI MTUPU"
 
Hiyo ni kwa mitandao yote mkuu. Salio unaloliacha sio hilo utakalolikuta kesho yake asubuhi. Airtel nadhan ndo hawaibi.
 
hiyo ni kwa mitandao yote mkuu. Salio unaloliacha sio hilo utakalolikuta kesho yake asubuhi. Airtel nadhan ndo hawaibi.

hii ni new infor. Kwangu. Kwa nini wanafanya hivyo? Nitacheki leo mitandao yote.
 
Kama umejiunga na huduma ya muito kwa mpigaji(caller tone)hayo makato yanahusika.mimi niliona ni upuuzi nikajitoa kitambo.sasa hv ukinipigia ni triiii.....triiii
 
Kama umejiunga na huduma ya muito kwa mpigaji(caller tone)hayo makato yanahusika.mimi niliona ni upuuzi nikajitoa kitambo.sasa hv ukinipigia ni triiii.....triiii

Mkuu unajitoaje hiyo miito kwenye Tigo na Airtel ,hata mi ishakuwa kero nataka nibaki na miito ya ngriiii ngriiii mi maimuna unasemaje?
 
Hiyo ni kwa mitandao yote mkuu. Salio unaloliacha sio hilo utakalolikuta kesho yake asubuhi. Airtel nadhan ndo hawaibi.
We yaani airtel ndio kabisa yaani mm sielewi kila siku nikiweka hela lzm nikute km 300 imekatwa nimejaribu kujitoa hadi kny huduma ya miito ya cm lkn wapi yaan nina hasira nao kweli ukija kny upande wa airtel money ndo usiseme yaan ni matatizo matupu!! Labda atleast kwa upande wa internet angalau wanajitahid
 
Nina laini ya airtel sitaipiga kwa leo. Najaribu hii kitu

Sasa hivi ni saa 08:07pm salio langu la airtel ni Tsh 808.
Nitakuja na salio langu kila nitakapojiskia mpaka tuone huo wizi.
Sijajiunga ktk huduma yeyote ya kipuuzi.
 
Hizi kampuni bana we acha, yaani ni wizi mtupu, mi hata sijui akina January wanafanya nini!
 
Kama umejiunga na huduma ya muito kwa mpigaji(caller tone)hayo makato yanahusika.mimi niliona ni upuuzi nikajitoa kitambo.sasa hv ukinipigia ni triiii.....triiii

Mkuu tusaidie namna ya kujitoa kwenye janga hili, mi niliingia mkenge ila sasa nataka kujitoa!!!
 
Hizi kampuni bana we acha, yaani ni wizi mtupu, mi hata sijui akina January wanafanya nini!

Kweli mukulu. TCRA wamekomaa na digitali na wanayaacha makampuni ya simu yafanye yatakavyo. Hakuna mwenye nafuu. Wote ni wezi tu.
 
Nina laini ya airtel sitaipiga kwa leo. Najaribu hii kitu

Sasa hivi ni saa 08:07pm salio langu la airtel ni Tsh 808.
Nitakuja na salio langu kila nitakapojiskia mpaka tuone huo wizi.
Sijajiunga ktk huduma yeyote ya kipuuzi.

NIMERUDI. Sasa hivi ni saa 06:37am ni siku nyingine 10/04/2013. Salio langu la airtel bado ni ile ile Tsh 808.
CONCLUSION: Inaonekana airtel hawaibi hivi vijisalio vyetu labda wizi mwingine. Hem volunteer mwingine wa tigo afanye lakini ambaye hajajiunga ktk hivi vihuduma vya kiseng.e sen.ge
 
Kama umejiunga na huduma ya muito kwa mpigaji(caller tone)hayo makato yanahusika.mimi niliona ni upuuzi nikajitoa kitambo.sasa hv ukinipigia ni triiii.....triiii

Mimi sijawahi kujiunga kwa kukwepa hayo mambo yao.
 
Tigo wamekata kwangu!!
 
Mkuu unajitoaje hiyo miito kwenye Tigo na Airtel ,hata mi ishakuwa kero nataka nibaki na miito ya ngriiii ngriiii mi maimuna unasemaje?

Tuma Ondoa kwenda 15050
 
Kama umejiunga na huduma ya muito kwa mpigaji(caller tone)hayo makato yanahusika.mimi niliona ni upuuzi nikajitoa kitambo.sasa hv ukinipigia ni triiii.....triiii

Nilivyokuwa najua mimi ni kuwa wanakata around 300 kwa mwezi kwa huduma ya hii.
 
weka na kutoa salio usiache simu ikiwa na salio hakikisha linasoma 0 kila siku
 
Mimi tigo walinitesa sana. Ilikuwa kila nikiweka 1000 na kuendelea wanalamba, nikataka kutupa line yao, but nikaamua kuwa sitoweka zaidi ya 500
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…