Nilikuwa mteja loyal customer wa Tigo, ulikuwa mtandao wangu wa kwanza lakini kwa sasa nimetokea kuichukia sana tigo natamani hata kuitupa line yangu ya tigo ili nisitamani hata kuitumia. Kwanza wanakata kiasi kikubwa ukilinganisha na wanachotangaza, pili kila huduma unayotaka kwao wanakata pesa eg ukimtumia hata mzazi wako pesa wanakata asilimia 0.3% ya pesa uliotuma. Hii inamaana wanakuchaji mara mbili, sielewi kwa nini wanikate wakati nimenunua credit ambayo naweza kuitumia kwa jinsi ninavyotaka. Tigo acheni kutafuta pesa kwa nguvu namna hiyo muwajali na wateja wenu..nashauri makato haya wayaweke kwenye matangazo yao ili mteja awe amejiandaa kuliko kama ilivyo sasa...wazo langu kwa TIGO.