tiGO mnatufukuza wateja wenu bila kujijua


Usijidanganye kuwa VODA ni nafuu.Jana nimemaliza buku kwa dakika 6 tu.Nadhani mitandao yote imeongeza gharama za kupiga simu
 
Mi huwa napenda kujaribu, muda huu nimepiga kwa majaribio na ni kama ifuatavyo;

nilikuwa na TShs 6258.90 nikaongea kwa sekunde 18 salio lililobaki ni TShs 6235.50 baadaya hizo sekunde 18 za maongezi, ukitoa jawabu ni TShs 23.40 nilizokatwa ambazo nikigawanya ni Tshs 1.28 sasa hii Tshs 3 imetoka wapi? Ngoja nijaribu tena kwenda simu nyingine.
 
Nimepiga tena na jawabu ni kama ifuatavyo;

nilikuwa na Tshs 6235.50 nimeongea dakika 1 na sekunde 08 ambazo ni sekunde 68, salio lililobaki ni Tshs 6147.10
nikitoa napata 88.40 nikigawanya ni Tshs 1.3, bado sijaona hiyo Tshs 3 imekatwa wapi hapa?
 
tigo ni noma, jamaa wanaendesha kampuni kihuni kweli, cjui vas na it dep. Wanasimamiwa na nani!!!?????!!!
 
Wana kurasa wao Facebook hawa. Jaribuni kutupia malalamiko pale!
 
Aisee wewe una bahati sana! Lakini ukweli ndo huo,tiGo wameongeza gharama za kupiga cm..

Nimepiga tena na jawabu ni kama ifuatavyo;

nilikuwa na Tshs 6235.50 nimeongea dakika 1 na sekunde 08 ambazo ni sekunde 68, salio lililobaki ni Tshs 6147.10
nikitoa napata 88.40 nikigawanya ni Tshs 1.3, bado sijaona hiyo Tshs 3 imekatwa wapi hapa?
 
hakuna mkweli katika makampuni yote!!! - na ndio ubepari ulivyo na hasa pale ufahamu wa soko (market information) kama unamnufaisha mtoa huduma au bidhaa - kunakuwa na unfair competition. TCRA au chombo kingine husika walitakiwa walione hilo na kuwa kama marefa - lakini wapi. hatma yetu watumiaji iko mikononi mwa haya makampuni ya simu - unakuwa na sim card 3 au zaidi - leo huku kesho kule ili mradi!!
 

Niko Rocky City, nimefika nikapokea sms kuwa pata salio mara 2 kila unapongeza salio, sijawai kuona kitu hicho zaidi naona inakula pesa kuliko laini nyingine, kwa maneno mengine ongeza salio ulipe mara mbili kupiga simu,

wanakera sana hawa jamaaa, nilishatupa laini yao, nimeikota tena, nikiitupa tena ndio kwaheri!
 
TiGO TIgo tiGO dah kweli nimewachoka mnavyofanya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…