Naandika nikiwa na uchungu sana. Mama yangu ana line ya tigo na amekua akiitumia siku zote na ameisajili. Kama siku mbili zilizopita, tukipiga simu yake imekua ikienda kwa mtu mwingine. Na huyo mtu amedai kwamba ameinunua hiyo number kutoka Tigo, ila ameshangaa kugundua kwamba ilikua ya mtu, na amekiri kupata usumbufu kwani mara nyingi amekua akipokea simu za mama.
Akadai kwamba atarudi Tigo kuwaeleza. Baadae simu ya mama ikawa haipatikani tena hewani. Kwa bahati, mama yupo hapa mjini (anaishi mkoani). Tuliamua kwenda Tigo (mlimani city) na kueleza tatizo tena baada ya kusubiri sana kwenye foleni. Walipoelezwa tatizo wakadai kwamba mama yangu atoe ID ili waweze kucheki.
Unfortunately hakua nayo, aliisahau kijijini, ila alikua na details za ile registration form. Waligoma kutoa msaada mpaka mama atoe ID. Kwa kweli imenimua kwani tatizo ni lao TIGO, kuuza number ya mtu ambayo inatumika na imesajiliwa, sasa wametusababishia usumbufu usio wa lazima.
Hivi nini maana ya ku register? Kwa nini wauze number kabla hawajacheki kama inatumika au la? Au kuna jambo ambalo sielewe? Wadau nisaidieni please.