tiGO mnatufukuza wateja wenu bila kujijua

Wamefanya kosa japo na nyie mngekuwa na ID usingeleta huu uzi.
 
Pole sana kijana kwa tatizo linalo mkabili mama pamoja na wale ambao wanawasiliana na mama yako.Hofu yangu ni kwamba kwa nini tgo waone shida kufanya hata temporary search ili kujiridhisha hata kidogo.Mwambie mama aende polisi kuripoti.
 
Pole sana kijana kwa tatizo linalo mkabili mama pamoja na wale ambao wanawasiliana na mama yako.Hofu yangu ni kwamba kwa nini tgo waone shida kufanya hata temporary search ili kujiridhisha hata kidogo.Mwambie mama aende polisi kuripoti.

sawa sawa....hawa tigo hawana maana ingawa marketing manager wao anajitahidi kujitetea humu jamvini_yaani huduma zao ni za hovyo kabisa.....anyway pole yake mama
 
Wapuuzi sana hawa tigo waliwahi kumpa namba ya demu wangu mtu mwingine nilifatilia mpaka basi ilibidi tuachane na tigo toka hiyo siku...
 
Apeleke lalamiko lake kwenye tume ya ushindani Tanzania akiwa na vielelezo vyote muhimu.
Atapa msaada na kurudishiwa gharama zake za usumbufu kama itabainika kutendewa kosa hilo.
Pole sana mama na kijana wako.
 
Nakushauri,
Hakikisha unaipata ID yako wanayoihitaji, fika na waonyeshe ili wathibitishe. Katika hili usiende kwa hawa customer care, WAAMBIE wakupe senior kwao ndio akusikilize. Kuwa imara na hakikisha unazo details zote za tangu line ilipokatwa mawasiliano yako. Wakikurejeshea, OMBA KUJUA NI NANI ALIYEIKATISHA MAWASILIANO YAKO.
Mwisho utaamu mwenyewe na sijui kama utatuletea feedbacks hapa jamvini, UWASHTAKI au UWASAMEHE kwa yote yaliyokusibu. Ila ukiwashtaki watakulipa pesa nyingi sana, tena kabla hujashtaki nenda katoe pia taarifa pale TCRA.
'Kazi ni kwako'.
 
Tigo imekuwa na gharama kubwa sana kwenye malipo ya vifurushi vya internet kuliko airtell. Wanafunzi wengi hasa wa chuo niwa tumiaji sana wa mtandao wa Tigo lakini kwa kuwa gharama za vifurushi kwa mwezi ni kubwa nimeshuhudia vijana wengi wakinunua kadi za airtell mtandao ambao kwa kifurushi chake ni shilingi 2500 tofauti na tigo wanakata shilingi zaidi ya 6000 kwa mwezi.
Tigo inakula kwenu taratibu.
 
Mkuu hiko kifurushi cha 2500 kwa mwezi kinakuwa ni cha simu au Kompyuta?
Na kinakuwa na kiasi cha Gb au Mb ngapi kwa kifurushi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…