TIGO sasa ile laki 8 yenu ya nivushe plus tumemalizana kiaina. Ngoja nisajili line ya YAS

Mnafikiri matumizi ya nida yalikuja bure tu..??
taarifa zako zipo mpk benki kama ulikuwa haujui hilo deni siku ukienda kukopa benki, benki husika wataangalia historia yako ya mikopo hapo ndipo watakapokosa uaminifu nawewe ndo utajua haujui!..
lipeni madeni yenu ya kwenye line za simu hizo ni cv.
 
Nchi inadawa kulikoni hizo bank
Kama ni hivyo nchi isingekopeshwa
 
Ukinyimwa mkopo benki shukuru.
Maana unachopewa na utakacholipa havina uhusiano hata kidogo.
Jamaa wa online loans waliniambia hutapata mkopo benki yoyote hapa nchini kwakuwa wananidai.
CRDB wakanipa pesa bila masharti
 
Kwamba imekula kwao?...walipe tu mkuu ili uweze kukopesheka zaidi kwani kimtindo hio mikopo ya mitandao husaidia pia
 
Ukinyimwa mkopo benki shukuru.
Maana unachopewa na utakacholipa havina uhusiano hata kidogo.
Jamaa wa online loans waliniambia hutapata mkopo benki yoyote hapa nchini kwakuwa wananidai.
CRDB wakanipa pesa bila masharti
mh! hivyo vikampuni vilivyofungiwa vilikuwa vinakutisha tu!.. nenda kwenye makampuni yaliyosajiliwa kihalali na BOT
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…