Aziz: Kampuni hii Kubwa ya TIGO
Hili sio pigo tu kwa tigo Bali pia kwa Serikali ya ccm kuanzi utawala wa mwenda zake mpaka huu wasamia wmekuwa na tabia ya kudukuwa mawasiliano ya watu. Huku wakijuwa ni kinyume cha katiba na sheria za nchi. Ipo siku watashitakiwa kama wadukuzi ndio watqjuwa kuwa sheria hazitugwi kwaajiri ya watawaliwa tu ,hata watawala zinawahusu.
Hamna kesi hapoTigo Tanzania PLC 😂😂😂
Afungue tu hakuna anayetishika wenyewe wenye brand name ya Tigo mabilionea mmojawapo huyo hapo tajiri wa dola na pesa za kigeni Rostam Aziz ana pesa kuliko huyo wakili wake Robert Amsterdam anayemtegemea Lisu huko uingereza aweza pambana na hiyo kesi popote dunianiMpaka sasa Lissu hajafungua mashtaka Rasmi. Hivyo endeleen kumpa madini asikwame. Angalau atapata pesa ya kununua gari kuliko kuomba omba
Unaelewa maana ya brand name wewe? BRAND name toka lini kisheria ikawa jina la kampuni?Hata kama sasa ni HONORA from MIC lakini TIGO ni ile ile.
TIGO Tanzania PLC 😄Hata kama sasa ni HONORA from MIC lakini TIGO ni ile ile.
Kampuni Tanzu 😂😂😂Unaelewa maana ya brand name wewe? BRAND name toka lini kisheria ikawa jina la kampuni?
Unaponunua Kampuni bila shaka unarithi madeni ya Kampuni mama husika. Kuna kila dalili kwamba HANORA inakiri kuwajibika kwa I'll responsibility za mmiliki wa awali. Ninaamini inayoshitakiwa na Tundu Lissu ni tiGo kwa hapa Tanzania na kwa London inayoshitakiwa na Michael Clifford ni Millcom na siyo tiGo kwa hiyo tiGo hawana jinsi yoyote ya kukwepa uwajibikaji huu kwa Tundu Lissu.Kampuni ya TIGO imesema haihusiki na sakata la kuvuja Taarifa za Tundu Antipas Lisu
HONORA imesema kampuni mama ya Tigo haikuwa mmiliki Wakati Makamu mwenyekiti wa Chadema mh Tundu Antipas Lisu anashambuliwa
----
Dar es Salaam. Kampuni ya Honora Tanzania Public Limited Company ("TIGO") imejitenga na taarifa za kuvujisha taarifa za simu za Makamu Mwenyekiti waChadema (Bara), Tundu Lissu, ikisema kampuni mama ya sasa ya Tigo haikuwa mmiliki wake wakati tukio lililoripotiwa.
Taarifa hiyo inatokana na kesi inayoendelea nchini Uingereza kati ya Kampuni ya Millicom iliyokuwa ikimiliki Tigo na aliyekuwa mfanyakazi wake, Michael Clifford ambaye sasa amefukuzwa kazi.
Kwa mujibu wa Gazeti la The Guardian la Uingereza la Septemba 24, 2024, Clifford aliwasilisha maelezo yake katika mahakama ya London kuwa, chanzo cha kufukuzwa kwake ni kutoa ripoti ya jinsi kampuni hiyo ilivyotoa taarifa za mawasiliano ya Makamu Mwenyekiti wa Chadema (Bara), Tundu Lissu.
Lissu alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 akiwa kwenye gari lake alipokuwa akielekea kwenye makazi yake baada ya kuhudhuria vikao vya Bunge jijini Dodoma.
Taarifa iliyotolewa la Honora Tanzania Public Limited Company leo Septemba 26, 2024 imeleza kutambua taarifa ya kesi inayoendelea nchini Uingereza ya ajira katika mahakama ya London inayomhusisha mfanyakazi wa zamani wa Millicom, kampuni mama ya Tigo hadi mwaka 2022.
Soma Pia:
- Tundu Lissu kuiburuza Tigo mahakamani
- Kupigwa risasi kwa Tundu Lissu: Kampuni ya simu ya Tigo yadaiwa ilivujisha mawasiliano yake kwa mamlaka
“Kampuni mama ya sasa ya Tigo haikuwa mmiliki wake wakati tukio lililoripotiwa lilipotokea,” imesema taarifa hiyo.
Imesema japo hawawezi kutoa maoni kuhusu undani wa kesi hiyo kwa kuwa hawahusiki moja kwa moja, bali wanahakikisha ulinzi wa taarifa za wateja wao.
“Tunataka kuwahakikishia wateja wetu na wadau wetu kwamba kulinda data zao binafsi kwa kuzingatia sheria na kanuni za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, bado ni kipaumbele chetu kikuu,” imesema taarifa hiyo.”
Chanzo: Mwananchi
We football Yako Mpira ya Sheria,waachie wenyewe,Aibu kubisha utumbo!Hamna kesi hapo
Wafute,wasifute kesi ya kujibu wanayo tuu!Kama walifuta wateja wote na kusajili upya sawa.
Kama huelewi maana ya brand basi kaa hivyo hivyoKampuni Tanzu 😂😂😂
Kujibu rahisi tu anayeshitaki ndie athibitishe hicho aongeacho dhidi ya tigoWafute,wasifute kesi ya kujibu wanayo tuu!
Brand ni kama " Kisungura"Kama huelewi maana ya brand basi kaa hivyo hivyo