tiGO wajitenga na sakata la kuvuja Taarifa za Tundu Lissu. Wasema mmiliki wa sasa ni mwingine si yule wa nyakati za shambulio!

tiGO wajitenga na sakata la kuvuja Taarifa za Tundu Lissu. Wasema mmiliki wa sasa ni mwingine si yule wa nyakati za shambulio!

KESI NI NGUMU SANA HII KWA UPANDE WA LISSU.

Tatizo linapokuja ni kwamba walioshitakiwa ni Millicom sio Tigo (Nimeatanisha attachments)

Taarifa za Lissu zilivuja kipindi ambacho kampuni mama inayomiliki Tigo ni "Millicom International Cellular public limited company"

Kuanzia mwaka 2022 kampuni mama mpya ni "Honora Tanzania Public Limited company"

Honora wataendelea kujibanza kwenye angle ya kumshinikiza Lissu aendelee kuwashtaki Millicom aliowafungulia kesi.inavyoonekana Millicom walivyoona ngoma inakaribia kupasuka wakaondoka mwaka 2022

Lissu ilibidi awashtaki Tigo kwasababu hata kampuni mama ikibadilika angeendelea kuwashtaki Tigo.
Nimemsikia mmoja akisema imeshitakiwa kampuni siyo wamiliki.
 
Kampuni ya TIGO imesema haihusiki na sakata la kuvuja Taarifa za Tundu Antipas Lisu

HONORA imesema kampuni mama ya Tigo haikuwa mmiliki Wakati Makamu mwenyekiti wa Chadema mh Tundu Antipas Lisu anashambuliwa
----
Dar es Salaam. Kampuni ya Honora Tanzania Public Limited Company ("TIGO") imejitenga na taarifa za kuvujisha taarifa za simu za Makamu Mwenyekiti wa Chadema (Bara), Tundu Lissu, ikisema kampuni mama ya sasa ya Tigo haikuwa mmiliki wake wakati tukio lililoripotiwa.

Taarifa hiyo inatokana na kesi inayoendelea nchini Uingereza kati ya Kampuni ya Millicom iliyokuwa ikimiliki Tigo na aliyekuwa mfanyakazi wake, Michael Clifford ambaye sasa amefukuzwa kazi.

Kwa mujibu wa Gazeti la The Guardian la Uingereza la Septemba 24, 2024, Clifford aliwasilisha maelezo yake katika mahakama ya London kuwa, chanzo cha kufukuzwa kwake ni kutoa ripoti ya jinsi kampuni hiyo ilivyotoa taarifa za mawasiliano ya Makamu Mwenyekiti wa Chadema (Bara), Tundu Lissu.

Lissu alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 akiwa kwenye gari lake alipokuwa akielekea kwenye makazi yake baada ya kuhudhuria vikao vya Bunge jijini Dodoma.

Taarifa iliyotolewa la Honora Tanzania Public Limited Company leo Septemba 26, 2024 imeleza kutambua taarifa ya kesi inayoendelea nchini Uingereza ya ajira katika mahakama ya London inayomhusisha mfanyakazi wa zamani wa Millicom, kampuni mama ya Tigo hadi mwaka 2022.

Soma Pia:

“Kampuni mama ya sasa ya Tigo haikuwa mmiliki wake wakati tukio lililoripotiwa lilipotokea,” imesema taarifa hiyo.

Imesema japo hawawezi kutoa maoni kuhusu undani wa kesi hiyo kwa kuwa hawahusiki moja kwa moja, bali wanahakikisha ulinzi wa taarifa za wateja wao.

“Tunataka kuwahakikishia wateja wetu na wadau wetu kwamba kulinda data zao binafsi kwa kuzingatia sheria na kanuni za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, bado ni kipaumbele chetu kikuu,” imesema taarifa hiyo.”

Chanzo: Mwananchi
Walinunua kampuni, wafanyakazi na madeni yake, wanachojaribu ni kutaka sisi tuwaamini.
 
Inayoshtakiwa ni Kampuni siô Mmiliki.
Hivyo Kesi bado Ipo palepale.

Nilitegemea Wakanushe kuwa hawakufanya hivyo lakini Kwa kauli yao inathibitisha kuwa kitendo kilifanyika na kilifanywa na Kampuni ya Tigo, semà Mmiliki ni Mwingine.

Jina la Kampuni NI lilelile.
Wateja wa Tigo na Namba za tigo ni zilezile ikiwemo Mhanga àmbaye ni Tundu Lisu

Hivyo Kesi Hapo bado yamoto.
Kwa kauli hii ya Honora ni wazi kuwa kuna jambo lilifanyika.
 
Kumbe baada ya mwaka 2019 walipoona kuna kesi imefunguliwa wakamuuzia Rostam Aziz akijiona yeye mwamba. Na mwezi wa April mwenyekiti wa millicon kajiuzulu kaona aibu itamkuta
 
Lissu akishawachota wafuasi wa CDM uwa awataki kusikia lolote.

Kwanza mzungu hajawai kuwa mwajiri wa TiGO Tanzania na wala hana ugomvi nao. Yeye alikuwa ni mwajiriwa wa Millicom U.K. LTD ndio maana ana mgogoro na kesi ipo kwenye employment tribunal huko kwao.

TiGO Tanzania awakutoa info bure bure isipokuwa kuna agent ya serikali ilitaka ipewe info za mteja (sasa kama walitumia sheria au la) maelezo hayo hakuna.

Mlolongo wote wa mzozo wao baina ya mzungu na mwajiri ilikuwa kuzuia kutaka nchi husika na mwanasiasa ambae communication zake zilikuwa zinapelekwa serikalini (Lakini si kwamba walikuwa wana track movement zake).

By now hiyo nchi inajulikana ni Tanzania na mwanasiasa mwenyewe ni Lissu. Waliobaki labda ni government agency na manager wa TiGO wa wakati huo.

It was just common sense kampuni ya simu aiwezi toa info za wateja wake kirahisi rahisi tu. Lissu tu na Amsterdam kukuza mambo.

Na kama Millicom walishauza TiGO ndio kabisa, labda na wenyewe hakina Lissu wakaishitaki hiyo Millicom.
 
Swali: Kama kampuni imeshida au kushindwa kesi kabla ya kuuzwa au ikiwa inaendelea na kesi alafu wamiliki wakabadilika nini kinafanyika? Kazi kwenu wataalam wa sheria.
 
Back
Top Bottom