tiGO wajitenga na sakata la kuvuja Taarifa za Tundu Lissu. Wasema mmiliki wa sasa ni mwingine si yule wa nyakati za shambulio!

tiGO wajitenga na sakata la kuvuja Taarifa za Tundu Lissu. Wasema mmiliki wa sasa ni mwingine si yule wa nyakati za shambulio!

Kampuni inapouzwa inauzwa na kila kitu chake kama ni madeni inadaiwa kama kuna jinai ilifanya basi kampuni inayonunua au watu wanaoinunua wanawajibika na jinai hiyo kwa muktadha huo basi TIGO hawakwepi hii kadhia lazima itakula kwao !!!!!!
 
Tundu Lisu: Tumepata pa kuanzia

Mbona unaogopa sana bwashee 😂
Hata kwenye mkasa wa kamanda Ally Mohamed Kibao ilikua hivi hivi tu, picha wakati linaanza wanaona na wanatoa taarifa chap chap, lakini pia picha wakati limeisha wanaona na wanatoa taarifa chap chap...

wakiulizwa,
jamani hivi kweli hapo katikatika hamjaona kulitokea au kilitendeka nini ati hawajaona kitu 🤣
 
Shujaa Ally Mohamed Kibao ni mbegu ya mabadiliko makubwa yanayokuja na yameanzia TIGO 🐼
 
Unaelewa maana ya brand name wewe? BRAND name toka lini kisheria ikawa jina la kampuni?

Kwahiyo ukifanya jinai ukabadili jina unakuwa ushaepuka jinai? Ndiyo unachotaka kusema? Kwani Lissu alikuwa anatumia line ya MIC au tigo?
 
Kampuni ya TIGO imesema haihusiki na sakata la kuvuja Taarifa za Tundu Antipas Lisu

HONORA imesema kampuni mama ya Tigo sio Makamu Wakati mwenyekiti wa Chadema mh Tundu Antipas Lisu anashambuliwa.
----
Dar es Salaam. Kampuni ya Hora Tanzania Public Limited Company ("TIGO") imejina na taarifa ya kuvujisha taarifa za simu za Makamu Mwenyekiti wa Chadema (Bara), Tundu Lissu, ikisema kampuni mama ya sasa ya Tigo haikutokea wakati tukio lililoripotiwa.

Taarifa hiyo inatokana na kesi inayoendelea nchini Uingereza kati ya Kampuni ya Millicom iliyokuwa imiliki Tigo na aliyekuwa waziri wake, Michael Clifford ambaye sasa amefukuzwa kazi.

Kwa mujibu wa Gazeti la The Guardian la Uingereza la Septemba 24, 2024, Clifford aliwasilisha maelezo yake katika mahakama ya London kuwa, chanzo cha kufukuzwa kwake ni kutoa ripoti ya jinsi kampuni hiyo ilivyotoa taarifa za mawasiliano ya Makamu Mwenyekiti wa Chadema (Bara), Tundu. Lissu.

Lissu alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 akiwa kwenye gari lake alipokuwa akielekea kwenye makazi yake baada ya kuhudhuria vikao vya Bunge jijini Dodoma.

Taarifa ya taarifa la Honora Tanzania Public Limited Company leo Septemba 26, 2024 imeleza inayobainisha taarifa ya kesi inayoendelea nchini Uingereza ya ajira katika mahakama ya Londonmhusisha wa zamani wa Millicom, kampuni mama ya Tigo hadi mwaka 2022.

Soma Pia:

“Kampuni mama ya sasa ya Tigo ilikuwa wake wakati tukio lililoripotiwa lilipotokea,” imesema taarifa hiyo.

Imesema japo hawezi kutoa maoni kuhusu undani wa kesi hiyo kwa kuwa hawahusiki moja kwa moja, bali wanahakikisha ulinzi wa taarifa za wateja wao.

“Tunataka kuwahakikishia wateja wetu kwamba tunalinda data zao binafsi kwa kuzingatia sheria na kanuni za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, bado ni kipaumbele chetu kikuu,” imesema taarifa hiyo.

Chanzo: Mwananchi
Hawaaminiki hawa.
Hata mimi nilipokuwa natafutwa na shemeji yangu walihusika kutoa mawasiliano yangu.
 
Kwahiyo ukifanya jinai ukabadili jina unakuwa ushaepuka jinai? Ndiyo unachotaka kusema? Kwani Lissu alikuwa anatumia line ya MIC au tigo?
Kampuni iliuzwa kwa mwingine na ikaondoka zake na kufunga biashara zake zote Tanzania. Tofautisha na kurithisa.Kampuni imeuza kila kitu na kufunga ofisi zao na biashata zao zote Tanzania na kufunga virago

Neno.kuu hapo kufunga biashara zake zote Tanzania kufunga ofisi na kuondoka nchini moja kwa moja

Hivyo hiyo Kampuni ya Milicon haipo tena Tanzania na walla haina bidhaa yake yeyote Tanzania inayoendelea kuuzwa .Hata kama kuna bidhaa inafanana jina na ile iliyokuwa ikiuza

Milicon hana bidhaa yeyote Tanzania anayouza.Tigo hii iliyopo sasa sio bidhaa ya Milicon na haina uhusiano nao tena ni bidhaa mpya ya mteja mpya aliyenunua biashara toka Milicon

Ukinunua suruali kwa mtu ukiivaa ile ile haiwi ya aliyekuuzia tena
 
Inayoshtakiwa ni Kampuni siô Mmiliki.
Hivyo Kesi bado Ipo palepale.

Nilitegemea Wakanushe kuwa hawakufanya hivyo lakini Kwa kauli yao inathibitisha kuwa kitendo kilifanyika na kilifanywa na Kampuni ya Tigo, semà Mmiliki ni Mwingine.

Jina la Kampuni NI lilelile.
Wateja wa Tigo na Namba za tigo ni zilezile ikiwemo Mhanga àmbaye ni Tundu Lisu

Hivyo Kesi Hapo bado yamoto.

Wamejibu kipuuzi puuzi tu...
 
Kampuni iliuzwa kwa mwingine na ikaondoka zake na kufunga biashara zake zote Tanzania. Tofautisha na kurithisa.Kampuni imeuza kila kitu na kufunga ofisi zao na biashata zao zote Tanzania na kufunga virago

Neno.kuu hapo kufunga biashara zake zote Tanzania kufunga ofisi na kuondoka nchini moja kwa moja

Hivyo hiyo Kampuni ya Milicon haipo tena Tanzania na walla haina bidhaa yake yeyote Tanzania inayoendelea kuuzwa .Hata kama kuna bidhaa inafanana jina na ile iliyokuwa ikiuza

Milicon hana bidhaa yeyote Tanzania anayouza.Tigo hii iliyopo sasa sio bidhaa ya Milicon na haina uhusiano nao tena ni bidhaa mpya ya mteja mpya aliyenunua biashara toka Milicon

Ukinunua suruali kwa mtu ukiivaa ile ile haiwi ya aliyekuuzia tena
Lissu anaishitaki Millicom(MIC) na GoTz ,hayo mambo ya Horona au tigo hayamuhusu! Maana case ya Misingi ni Clifford anaishitaki Millicom kwa unfair termination.
 
Kampuni ya TIGO imesema haihusiki na sakata la kuvuja Taarifa za Tundu Antipas Lisu

HONORA imesema kampuni mama ya Tigo haikuwa mmiliki Wakati Makamu mwenyekiti wa Chadema mh Tundu Antipas Lisu anashambuliwa
----
Dar es Salaam. Kampuni ya Honora Tanzania Public Limited Company ("TIGO") imejitenga na taarifa za kuvujisha taarifa za simu za Makamu Mwenyekiti wa Chadema (Bara), Tundu Lissu, ikisema kampuni mama ya sasa ya Tigo haikuwa mmiliki wake wakati tukio lililoripotiwa.

Taarifa hiyo inatokana na kesi inayoendelea nchini Uingereza kati ya Kampuni ya Millicom iliyokuwa ikimiliki Tigo na aliyekuwa mfanyakazi wake, Michael Clifford ambaye sasa amefukuzwa kazi.

Kwa mujibu wa Gazeti la The Guardian la Uingereza la Septemba 24, 2024, Clifford aliwasilisha maelezo yake katika mahakama ya London kuwa, chanzo cha kufukuzwa kwake ni kutoa ripoti ya jinsi kampuni hiyo ilivyotoa taarifa za mawasiliano ya Makamu Mwenyekiti wa Chadema (Bara), Tundu Lissu.

Lissu alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 akiwa kwenye gari lake alipokuwa akielekea kwenye makazi yake baada ya kuhudhuria vikao vya Bunge jijini Dodoma.

Taarifa iliyotolewa la Honora Tanzania Public Limited Company leo Septemba 26, 2024 imeleza kutambua taarifa ya kesi inayoendelea nchini Uingereza ya ajira katika mahakama ya London inayomhusisha mfanyakazi wa zamani wa Millicom, kampuni mama ya Tigo hadi mwaka 2022.

Soma Pia:

“Kampuni mama ya sasa ya Tigo haikuwa mmiliki wake wakati tukio lililoripotiwa lilipotokea,” imesema taarifa hiyo.

Imesema japo hawawezi kutoa maoni kuhusu undani wa kesi hiyo kwa kuwa hawahusiki moja kwa moja, bali wanahakikisha ulinzi wa taarifa za wateja wao.

“Tunataka kuwahakikishia wateja wetu na wadau wetu kwamba kulinda data zao binafsi kwa kuzingatia sheria na kanuni za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, bado ni kipaumbele chetu kikuu,” imesema taarifa hiyo.”

Chanzo: Mwananchi
TIGO inawezaje kuikana TIGO.
 
Hata kwenye mkasa wa kamanda Ally Mohamed Kibao ilikua hivi hivi tu, picha wakati linaanza wanaona na wanatoa taarifa chap chap, lakini pia picha wakati limeisha wanaona na wanatoa taarifa chap chap...

wakiulizwa,
jamani hivi kweli hapo katikatika hamjaona kulitokea au kilitendeka nini ati hawajaona kitu 🤣
Acha uzushi wewe!!
 
Wewe ndiye unayetuhumu ndiyo unatakiwa kuthibitisha.
sina haja kutuhumu chochote kwenye hili, ispokua naona mazingira ya kujihesabia haki kwa mbwembwe sasa kwenye hili, na hivyo nadhani ingependeza zaidi picha la katikatika likawekwa wazi na wa husika itasaidia sana kuona kama wanahusika au hawahusiki 🐒
 
Hueleweki.

Unataka kusema nini?
 
Back
Top Bottom