makilo
JF-Expert Member
- Dec 15, 2015
- 2,620
- 5,260
Kheri ya ijumaa kuu kwa wote.
Siku ya tarehe 23 mwezi wa 3,nilifanya malipo kwa njia ya mtandao nililipa ticket ya bus Dar to Mwanza.
Malipo yangu hayakufanikiwa nikawasiliana na huduma kwa wateja wakaniambia kuna tatizo la kimtandao kwa hiyo fedha zangu zitarudishwa baada ya siku 3.
Kila baada ya siku tatu nikawa nawakumbusha ikaanza story ya masaa 24 nitarudishiwa changu, nikaona niende Makao Makuu Makumbusho nikaambiwa wameshachukua taarifa zangu hivyo nitarudishiwa baada ya saa 24.
Nimekaa siku 2 nimewapigia wanasema mbona huku tumeshakurudishia? Jamani jamani jamani TIGO wamekuwa na huduma mbovu mbovu mno.
Nikarudi Tena makao makuu wakaniambia niwawie radhi pesa yangu bado inaonekana ipo kwao nikae baada ya siku 3 itakuwa mikononi mwangu. Juzi jumatano nikawapigia kuuliza Mana siku 3 zimekata nikaambiwa masaa 24 nisubiri nikabakia kucheka tu.
Leo nawapigia simu kwa number Yao ya 100 inapokelewa ila upande wangu si sikii chochote wamenipiga "MUTE" maana nikitumia simu ya mtu mwingine wanapatikana vizuri tu.
Wakuu nahitaji changu jasho langu sio vyema likapotea kirahisi rahisi.