Tigo wanashirikiana na matapeli kutapeli mawakala wao?

Nimeongea na tigo huduma kwa wateja eti wanasema "ulichukuq kitambulisho cha aliyetoa pesa" wtf!!!
Hivi kweli mtu amekuja na line yake na namba za siri zake unasema mpaka atoe kitambulisho? Hata kama ni utaratibu kiukweli hayo sijawahi ona mahali Tanzania hii mtua huduma za mtandao anadai kitambulisho ili mteja atoe pesa.
Nikiwauliza kwa nini mlirudisha pesa kwa mteja aliyetoa pesa, hawana majibu. Maana yake sasa hivi kila mtu atatoa pesa kwa wakala then after a couple of minutes atasema haujui muamala atasitisha na atarudishiwa pesa zake, sasa hapa usalama wa hii biashara upo wapi?
Tutaacha hii biashara kama watoa huduma ni sehemu ya wezi!!
 

Ww sio wa kwanza kuna mtu huku alitoa pesa 300k kwa wakala kisha akaomba muamala urudishwe baada ya dkk 50+ na kumbe aliyetoa alituma namba kwabm2 mkoani akifanya kama anatoa na kumbe aliyetoa yuko mkoani. Sasa yule wakala akabadirisha ile hela kwa wakala mkuu akapata mtandao mwingine. Ile baadaye anaona txt muamala fulani umezuiwa na mtoaji ameomba urejeshwe wkt huo account ya tigopesa ya wakala ikiwa na elf 12 hv. Basi tigo ikalamba ile 12k kishaikafunga namba ya wakala haipokei simu na anaambiwa bado anadaiwa, sms zinamfikia ila eti simu wamefunga kwa huyu wakala.

Sasa najiuliza
Muamala uliotolewa ni 300k, ila tigo wamechukua 12k ambayo ni salio la wakala. Kwanini wafunge wakala line yake isipokee simu, 2kwanini wasitume ujumbe wakala kwenda kuripoti.

Kwa hesabunza haraka huyu wakala ilikuwa aliwe 312k ila kwakuwa ile 300k tyr alikuwa ameshaitoa tigo wakaamua kumchomolea 12k . Tuseme wakala katapeliwa 12k kutoka katika muamala wa 300k kwa ushirikiano wa tigo na matapeli wa2.
Biashara ya tigopesa kumbe ni ngumu
 
UsiendenTCRA nenda bot wao ndio wanatoa leseni za huduma za kifedha.
 
Mi nitaachana na tigo pesa. Sijui mamlaka hazioni hii loophole ya wizi inayofanywa na tigo? Muamala uliotolewa kwa wakala usirudishwe mpaka wakala apigiwe aitwe akatoe scenario ya huo muamala. Sasa matapeli wanaonekana kuwa na upper hand kwa kusaidiwa na Tigo
 
Fatilia mkuu mpaka mwisho
 
 

Attachments

  • FB_IMG_1727368868627.jpg
    57.3 KB · Views: 5
mimi nilikuwa na laini yatigo,lakini nimeachana nayo!!
 
Kama Maelezo ya mlalamikaji yako sawa, basi hawa Yas wajitathimini vizuri. wasije wakaharibu jina, uaminifu na biashara yao kwa Mawakala na sisi wateja wao. Kama wakala analalamika, je! sisi wateja si ndio tutapigwa tukose pa kuhemea?

Yas mje na majibu/maelezo ya kina kwenye hiii tuhuma. Wakala kashasema kuwa, huduma imefanyika within the same range. na Muamala ukasitishwa makusudi na Mteja ambaye sio mwaminifu, huku wakala akiwa tayari keshatoa huduma ya Cash kwa mteja. hii inaleta sintofahamu. hii ukimpata Mwanasheria mzuri, mbobezi kwenye Civil cases(Kesi za madai) utalamba hela nzuri kama akina Mwana FA na mwenzie walivyoishinda TIGo by then kwa kutumia nyimbo zao kwenye miito bila ridhaa yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…