Tijikumbishe: Ronaldo De Lima alikumbwa na nini Fainali ya Wold Cup 98

ESCORT 1

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2015
Posts
1,412
Reaction score
3,043
Ni mkasa wa aina yake, dakika kadhaa kabla ya mchezo wa fainali ya kombe la dunia mwaka 1998 pale nchini Ufaransa, katika mechi iliyokuwa inazikutanisha Ufaransa Vs Brazil kulitokea tukio la kushangaza sana.

Mshambuliaji bora wa wakati huo, Ronaldo De Lima alipatwa na ugonjwa wa ghafla na kuondolewa kwenye kikosi cha kwanza.

Dakika kadhaa baadae, akapata nafuu akapangw ingawa inaaminika alifosiwa. Kwenye fainali akawa mdembwedo kweli. Mpaka leo kuna nadharia nyingi juu ya tukio hilo. Je nini hasa kilimkuta Ronaldo?
 
Wanasema Alipata "gedegede" aah!!!! Alipata degedege

Wengine wanadai france walifanya yao..

Wengine wanasema Adidas walifanya yao ili zizzou ambae alikuw chini ya adidas annyanyue ndoo.
Hii inakuja kwa nguvu ya ushindani wa biashaka kati ya nike(mdhamini wa ronaldo de lima) na adidas(mdhamini wa zinedine yazid zidane, zizzou)
 
Kwani baada ya hapo Brazil walikutana Mara ngapi na zote wakawa wanapigwa tuu?
 
Hakuna uchawi, brazil alizidiwa mpira na ufaransa by then na pia ile ni fainali lengo ni ushindi ndicho walichokifanya ufaransa. Hata leo bado kuna watu hawaamini Barcelona alichezea kichapo toka kwa Liverpool. HUO NDIO MPIRA, unaweza kuwa na the best people lakini ukakosa mbinu za kuwin mechi fulani tena mechi muhimu
 
What happened 2002? Si kilikuwa ni kizazi hicho hicho? And then 2004?

2004 hujui alichomfanya Mwingeleza dak za 90 au unajisahaulisha magoli ya Zizou?

Kijana kubali kataa kile kizazi kilikuwa bora

Worldcup 98
Euro 2000
Euro 2004
World cup 2006

Miaka hiyo yote nane kizazi kile kilikuwa bora
( iv unakumbuka 2006 France ilikuwa na no 9 ( kumi na 6 kati yao wakiwa wanaongoza ufungaji bora kwenye league wanazocheza? Mpk kocha anashindwa nan wa kupangwa?)

Labda kama umeanza kuangalia mpira juzi but kizazi cha Zidane/Thuram/Lizarazu/Deschamps/blanc etc kilikuwa bora sana
 

Mbona umeiruka 2002 ambapo walikuwa kundi na Senegal?

2004 wametolewa na Greece, hope unakumbuka pia hilo swala.

Kwangu mimi France ilikuwa ya Euro 2000.
 
Mbona umeiruka 2002 ambapo walikuwa kundi na Senegal?

2004 wametolewa na Greece, hope unakumbuka pia hilo swala.

Kwangu mimi France ilikuwa ya Euro 2000.
Euro 2000 ilitwaa kwa Aina yake tuu ile mechi ya final wanasubir Hadi David Trezeguet asawazishe....ila alipita kwa shida maana Nusu final tuta la dakika za mwisho la Abel Xavier ananawa mpira ila 98 wanshinda kiulaini Sana kwakua Brazil alizidiwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…