SI KWELI Tiketi za Simba day ziliuzwa kwa mafungu na ulanguzi ili ziishe mapema

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Kwa mujibu wa Haji Manara Simba waliwatuma watu wanunue tiketi kwa mafungu ili waje wazilangulishe siku ya mechi ili watabgaze Sold out, asena sold out ya Simba ni ya mchono.


Nachojiuliza taarifa hiyo ni kweli? Kama kweli Simba watakuwa wanadanganya ili iweje?

Your browser is not able to display this video.
 
Tunachokijua
Simba Sports Club ni klabu ya soka yenye makazi yake katika kata ya Kariakoo katika Wilaya ya Ilala Mkoa wa Dar es Salaam nchini Tanzania.

Simba Ilianzishwa mwaka wa 1936, Jina la utani ni Wekundu wa Msimbazi (Wekundu wa Msimbazi), ni kumbukumbu ya watani wao wote wenye wekundu hao na Mtaa wa Msimbazi uliopo Kariakoo yalipo makao makuu yao.Simba ni moja ya klabu yenye Wingi wa mashabiki na moja kati ya klabu kubwa nchini Tanzania.

Simba imemaliza kuweka kambi nchini Misri ambako ilikuwa ikijiandaa na msimu mpya wa Mashindano 2024/2025 ambapo imerejea nchini Julai 31, 2025.

Katika siku hiyo hiyo ya Julai 31 2024 Simba SC iliweka chapisho katika mtandao wa X kuwa uuzwaji wa Tiketi za kwenda kwenye tamasha la Simba Day limefika tamati kwani tiketi zote 60000 za uwanja wa Benjamini Mkapa zimekwisha kununuliwa zote.

Baada ya chapisho hilo zilizuka hoja kuwa Simba imetoa taarifa isiyo ya kweli kwani mfumo bado unaruhusu kununua tiketi ivyo taarifa yao ya kuuzwa kwa tiketi zote si ya kweli.
Je, ukweli ni upi?
Baada ya kuibuka hoja hizo mdau wa Jamiicheck ametaka kufahamu ukweli kuhusu jambo hili, JamiiCheck imefuatilia madai hayo. JamiiCheck imewasiliana na Meneja wa Oparesheni wa Kituo cha Taifa cha Kuhifadhi Data (NIDC), Nasra Mugheri ambaye amesema kuwa Tiketi za Tamasha la Simba zimeisha siku ya Julai 31, 2024 sawa sawa na tarehe ambayo Simba walitangaza Sold out na mfumo wao hauruhusu kununua tiketi kimafungu kama inavyodaiwa.

Aidha, Ncard wamebainisha kuwa mfumo wao umeshafunga zoezi la kununua tiketi za Tamasha la Simba sababu zimeshaisha, maneno na hoja zinazoendelea ni maneno ya kishabiki.

Hivyo, kutokana na kanusho la N-card juu ya madai ya tiketi kununuliwa kimafungu na mfumo wa N-card kuendelea kuuza tiketi Jamiicheck imejiridhisha kuwa Madai ya Haji Manara na wengine ni ya uzushi.
Hivi huyu jamaa sijui anakuwaga na akili gani ???
 
Jamiiforum mko biased sana, habari za makolo mnazifanyia kazi haraka na kukanusha ila habari za Wananchi kama ile ya mzize kugomea mazoezi mmekaa kimya hamtaki kuikanusha, masaburi yenu.
 
Jamiiforum mko biased sana, habari za makolo mnazifanyia kazi haraka na kukanusha ila habari za Wananchi kama ile ya mzize kugomea mazoezi mmekaa kimya hamtaki kuikanusha, masaburi yenu.
Habari Mkuu,

JamiiCheck inafanya uhakiki wa taarifa za nyanja zote kwa usawa bila kubagua. Ikiwa kuna taarifa unahitaji ifanyiwe uhakiki tafadhali ianzishie uzi itafanyiwa kazi kwa haraka iwezekanavyo

Asante
 
Kuna video inasambaa mtandaoni imepostiwa na Haji Manara ikionesha mashabiki wa simba wakinunua tiketi kwenye ofisi za Simba kariakoo. Manara kathibitisha kua alizungumza ukweli kwamba sold out ni uongo
Your browser is not able to display this video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…