Tafuta habari kwenye chanzo cha kuaminika mkuu acha kukurupuka
Sasa goal.com sio chanzo cha kuaminika? Okay chanzo chako wewe kipo wapi? Vipi ni reputable?
Tiketi zinazo tajwa hapa ni scalping au resale.
FIFA wanapotangaza bei ya tiketi huwa bei inakuwa cheap, kuna mashabiki au watu hujitokeza kununua tiketi kwa wingi na kutengeneza uhaba kwa sold out.
Kwa hiyo mashabiki wakitaka kununua tiketi kwenye mfumo wanaambiwa tiketi zimeisha.
Halafu baada ya kuzoa tiketi hizo, wanaziamishia kwenye online market mitandao maarufu kule Amerika ya uuzaji tiketi ni
TickPick na
StubHub na kuziweka kwa bei ya juu sana (hadi $2,950) ili wapate faida kubwa ya haraka kutoka kwa mashabiki waliokata tamaa ya kukosa tiketi za FIFA.
Mpango wao ulikuwa unaenda fresh na ukiwalipa faida za juu lakini baada ya Portugal na USA kutolewa. Automatically watu waliokuwa tayari kutoa pesa nyingi kwa ajili ya mechi ni kama walipoteza hamu.
Kwa hiyo demand ilipopungua na wao wamebaki na maelfu ya tiketi kwenye stock, iliwalazimu washushe bei kwa zaidi ya 60% ($1,200) baada ya kuogopa kupata hasara.
FIFA wanataka watu wanunue tiketi moja kwa moja kwenye vyanzo vyao na kama itatokea hatahudhuria mechi wanasema tiketi irudishwe ili iende kutumiwa na shabiki mwingine.
Lakini kwasababu hayo makampuni ya uuzaji tiketi yapo Marekani ambapo sera za nchi zinaruhusu, FIFA anabaki hana la kufanya.
Hii ni sawa na watu wanaoenda kucheki mechi kwa Mkapa ikiwa masaa machache ticketi zimetangazwa kuisha lakini wanaenda wanafika getini wanasikia mtu anauza tiketi ya mzunguko shilingi 20K wakati bei halisi ni 5K
Sasa kwa Marekani hii ni biashara ambayo ipo rasmi kabisa na makampuni yanayofanya hivyo yamesajiliwa kihalali.