Yoyo Zhou
Senior Member
- Jun 16, 2020
- 126
- 215
TikTok ni mtandao wa kijamii wa video unaomilikiwa na Kampuni ya Bytedance ya China. Kutokana na teknolojia yake ya hali ya juu, mtandao huo umewavutia watumiaji milioni 170 nchini Marekani katika miaka michache iliyopita, ambayo ni nusu ya idadi ya watu nchini humo. Aidha, mwaka jana pato la TikTok nchini Marekani lilizidi dola bilioni 16 za Kimarekani. Baada ya hapo, baadhi ya wanasiasa wa Marekani waliinua fimbo yao, wakidai kwamba TikTok ina data nyingi za watumiaji, na “inatishia usalama wa taifa”, hivyo ni lazima “hatua kali” zichukuliwe. Lakini TikTok imeeleza kwamba inafuata sheria zote za Marekani, na kuahidi kuhakikisha usalama wa data, na hata inakubali kujiweka chini ya uchunguzi mkali wa serikali ya Marekani. Hata hivyo Marekani haitaki kuisamehe, na hadi sasa imetoa amri ya kuipiga marufuku mara mbili.
Wakati serikali ya Marekani inapiga kampeni ya kuimaliza TikTok, wanasiasa wa nchi hiyo wamefungua akaunti zao kwenye mtadano huo bila ya kusita, kwani wanajua TikTok ni chombo kizuri cha kuwavutia wapiga kura katika uchaguzi.
Habari zinasema kwenye video ya kwanza iliyotolewa na Trump baada ya kufungua akaunti kwenye TikTok, Mkurugenzi Mtendaji wa Michezo ya Fainali ya Mapigano (UFC), Dana White, ambaye aliandamana na Trump, alisema: “Rais sasa anatumia TikTok.” “Ni heshima yangu.” Trump akajibu. Licha yake, Kamati yake Kisiasa “Make America Great Again” pia imejiunga na TikTok, ili kumsaidia kuwavutia wapiga kura vijana.
Hata hivyo, wakati Trump alipokuwa madarakani, aliitendea vibaya mtandao huo wa TikTok. Mwaka 2020, alisaini amri ya kuipiga marufuku TikTok, lakini mwishowe alishtakiwa na TikTok, na kufuta amri hiyo kutokana na hukumu ya mahakama.
Kama Trump, Rais Biden pia anaipenda na kuitendea vibaya TikTok. Alifungua rasmi akaunti ya TikTok Februari lakini miezi miwili baadaye, alisaini rasmi muswada wa kulazimisha ByteDance kuacha TikTok, ama sivyo, TikTok itapigwa marufuku kabisa nchini Marekani.
Marekani inadai kuwa inaheshimu uhuru wa kutoa maoni, na ni soko huria zaidi duniani. Lakini katika suala la TikTok ambayo ni APP halali iliyoanzishwa kwa kufuata sheria na utaratibu wa nchi hiyo, imeacha maadili yote, na kufanya kama jambazi anayetaka kuiba kitu kizuri cha watu wengine.