TikTok itafungwa

TikTok itafungwa

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2020
Posts
620
Reaction score
1,240
TikTok itafungwa 2025

images (31).jpeg


TikTok itakutana na rungu nchini marekani ifikapo January 2025 itakua mwisho kutumika nchini marekani. Ikiwa byte dance atashindwa kuuza hisa zake kwa wamarekani.

Karatasi aliyotia sign raisi wa marekani Biden kuwapa muda wachina waliounda app ya TikTok siku 270 kuweza kuuza hiyo app Yao ikiwa watashindwa basi itafungiwa kabisa kutumika marekani.

Itaweza kuweka kizuizi kwa watu wa marekani kuweza kupakua hiyo app na kutumia maamuzi hayo aliyafanya siku ya jumatano na kusema mwisho wa kutumia app ya TikTok marekani ni 19 januari 2025.

Hata hivyo Biden amesema anaweza kuwaongezea siku zingine 90 ikiwa wataonyesha nia ya kutaka kuiuza hiyo app ikiwa watakahidi basi hiyo app itaondolewa kwenye soko la American app store hivyo mtu aliyoko marekani hatoweza kamwe kutumia app ya TikTok.

#tiktok #tiktoktanzania #tiktokbanned
 
Wamarekani wana ubabe wa kipumbavu sana. Hawataki maendeleo ya wengine
Kutukana hovyo ni dalili ya kukosa akili. Ukiona unapenda kutukana sana, ujue kichwani hakupo sawa.

Ungesoma vizuri, uelewe kabla ya kuanza kutoa maneno ya kashfa. Hao Wamarekani, kama Serikali yao itachukua hiyo hatua, ni dhahiri serikali yao itakuwa inaongozwa na watu wenye akili sana, watu wanaowajali watu wao.

Marekani haijaizuia Tiktok kufanya biashara Marekani, lakini wanataka wananchi wao, ambao ndio wateja wa hiyo Tiktok, ambao ndio watakaoitengenezea faida Tiktok, nao washiriki kwenye sehemu ya faida wanayoitengeneza. Yaani Tiktok ijiandikishe kwenye soko la hisa la USA, ili nao waweze kununua hisa.

Kama hujui, Wachina wanawazuia watu wao kutumia Whatsapp. Ukipatikana unatumia, ni kosa, unaadhibiwa!! Hilo hulishangai?

Saudi Arabia, ukiwekeza mradi wako wowote, ni lazima ushirikiane na wasaudia, hilo hulishangai?

Nchi zinazjitambua, zilizobahatika kuwapata watawala wenye akili, wanaotaka wananchi wao wafaidike na chochote wanachochangia kukinawirisha, ndivyo wanavyofanya.

Nchi zinazoongozwa na viongozi waliokosa uelewa na wasiojali wananchi wao, kama wa hapa kwetu, mgeni anaweza kuja, anaanzisha kampuni ya kuvuna rasilimali, na wala hauzi hisa hapa kwetu, lakini anauza hisa Toronto Stock Exchange, Sydney Stock Exchange, London Stock Exchange; huku watanzania wakiwa hawana habari, wanashindana namna ya kumsifia mama!!!
 
Itafungwa Marekani nchi zingine itaendelea
 
Back
Top Bottom