Tiles zimepanda bei

Billie

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2011
Posts
13,588
Reaction score
22,752
Aisee niliulizaga hizi tiles za 40x40 ili nimalizie ujenzi nimekuta zimepanda bei nikauliza nini sababu muuza duka akanijibu WANATOZWA KODI KUBWA.HILI JIBU LIMENISIKITISHA SANA AISEE NIMESHANGAZWA NA HII SERIKALI INAVYOJITANABAISHA KUWA NI WA WANYONGE sasa sijui hao wanyonge ni wa MALAWI au TZ.
 
Gharama za maisha tu hizo mkuu hakuna namna
 
Uliuliza kodi ya kitu gani? Inawezekana ni kodi ya pango.
 
Hutaki mlipe kodi hivyo vituo vya afya, barabara na reli mnajenga na nn?
 
Kwa kweli mi niliuliza mwezi uliopita ikabidi nikajipange ili nije kununua nineshangazwa kukuta imepanda tena imenibidi nipige hesabu ya sakafu ya kawaida iliyobaki nimeenda bar hadi sasa nipo napoza machungu.
Mkuu wachina wamejenga viwanda vingi sana vya tiles Dar es salaam lakini cha ajabu bei ya tiles inazidi kwenda juu kila kukicha..
 
Tulipishwe kodi lakini sio za kuumizana wanampandishia mwenye kiwanda na yeye anashusha kwa mtumiaji wa mwisho na hapo hapo serikali inafail kuonekana inamjali mnyonge.
Hutaki mlipe kodi hivyo vituo vya afya, barabara na reli mnajenga na nn?
 
Uliuliza kodi ya kitu gani? Inawezekana ni kodi ya pango.
Muuza duka kasema kiwandani huko wamepandishiwa kodi na serikali sasa mi sijui.Kodi ni kodi tu hata kama ingekuwa ya premises inaathiri bei pia.
 
Zile za Tanga vipi wanazouza barabarani?
Naona tutatumia hizo
 
Kwa kweli mi niliuliza mwezi uliopita ikabidi nikajipange ili nije kununua nineshangazwa kukuta imepanda tena imenibidi nipige hesabu ya sakafu ya kawaida iliyobaki nimeenda bar hadi sasa nipo napoza machungu.
Zimepanda kutoka bei gani hadi bei gani?
 
Kuna mtu atakuja na comment hii 'TUSHAJUA UNAJENGA'
 
Kuna kiwanda kipo Mkuranga kikubwa sana.Kuna mfanyakazi nilikuwa naongea naye akasema hapa kuna tiles nyingine zinatengenezwa zinaenda kuuzwa china nkabaki kushangaa.
 
Tiles hazijapanda bei. Umeenda maduka mangapi na upo mji gani?
Hakuna kodi mpya hadi sasa.
Fikiria maneno yako ya uwongo.
 
Kama ulishindwa kujenga kipindi kikwete yupo kwa sasa kalewe tu au usubiri aondoke..alisema mtaishi kama mashetani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…