Till you love yourself... Inawezekana?

Mie nakubaliana na huo msemo... Nikiwa kama mwanamke I understand hio statement more than a man can ever understand. Kuna watu (sio wanawake pekee thou wanashika dimba); wana low self esteem hadi balaa! Na kama una Low self esteem loving yourself ni mtihani sana.

Hii mara nyingi wahanga wa hii ni mabinti hasa katika young age ambayo mara nyingi wanakuwa hawajiamini katika kila kitu, iwe miili, jamii ama peer groups. Kujisikia vizuri mara nyingi kwao huegemea mtu ambaye yupo worse than her.. (Mfano kama ni mzuri akawa kazungukwa na wasichana ambao sio wazuri kama yeye inamuongeza self confidence; na iwapo awe katika kundi ambalo yeye anaokana ni the least beautiful basi anakuwa down... Sad, but in most cases true). In such case kuna explanition moja tu! (You don't love yourself enaf... sababu if you do, hakuna ambae anaweza kukufanya ujisikie tofauti no matter what). Take note; huo ni mfano tu sio kwamba basis of not loving oneself zote zipo hapo...

Wengine hadi wanakuwa watu wazima bado they don't love themselves enaf... Hapo ndipo hasa ukikutana na mtu ambae anakutambua, akaelewa weakness zako hasa hio ya kutojipenda hukusimamia na kuhakiksha you overcome that. To me hio statemet makes PERFECT sense...
 

But mpaka mtu apate bahati hiyo sio mchezo
most wanapata watu wa kuongeza to 'dislike themselves
 
This is very true. . it even apply kwa manaopendana. . mke mume yani mume wangu anavozidi kunionyesha upendo najipenda nasikia raha confi inaongezeka. . hata asiependeka atakubali hata kimyakimya. .
 
Japo sijawahi kuusikia huo wimbo na wala siujui ila hayo maneno ni wazi kuwa yanamzungumzia mtu aliyekata tamaa katika mapenzi na aamini tena juu ya mapenzi.

Ni kweli mtu aliyepoteza imani na mapenzi ni ngumu kujipenda mwenyewe na wala kujali sana juu yake....

Kuna mifano ya kifasihi simulizi nyingi jinsi mtu alivyojisusa baada ya kupoteza aliowapenda na alioamini wanampenda...

Hali hii imepelekea watu hawa kutokujali sana juu ya penzi jipya, na wengi huanza kujenga falsafa kuwa hamna kitu kinachoitwa "penzi la kweli"

Hivyo ni kweli kuna watu wanafikia hali hiyo Mkuu wangu The Boss....

Inawezekana kuwarejesha watu hao kwenye mwanga wa mapenzi japo ni shughuli pevu sana na inataka kujitoa muhanaga sana....
Binafsi ilishanishindaga mara kadhaa.......lol
Ni kazi ya hatari sana sababu unaweza ukajikuta na wewe unauokota huo ugonjwa wa kutokuamini kwenye mapenzi
 
Last edited by a moderator:
....nimejifunza kupenda, nijipende mimi kwanza... Hayo ni maneno ya grace matata. Mi naona upendo unaanzia kwako mwenyewe, kama unajipenda utajijali na kuweza kujifanyia yale mazuri. Mtu anayejipenda ni rahisi hata kuonesha upendo kwa wengine, ni rahisi kuweza kufanya yale yanayompendeza yeye kwa wengine iwapo hatokuwa mbinafsi. The boss kama moyo wako umetawaliwa na upendo ni rahisi pia kuwavutia watu wakupende.
 

Hii kazi inawashinda wengi aisee
 
This is very true. . it even apply kwa manaopendana. . mke mume yani mume wangu anavozidi kunionyesha upendo najipenda nasikia raha confi inaongezeka. . hata asiependeka atakubali hata kimyakimya. .


It works for u i guess..
 

Nitautafuta huo wimbo...aisee
 
hapo kwa red, kama ulivyosema wewe unaamini, lakini naweza kukuambia kuwa kuna watu wanajua kupenda kiasi kwamba hata kama ulikuwa unajichukia utagundua kuwa kuna love.
tukija kwenye mada, mimi naamini kuna kupendwa mpaka ukajipenda. unajua watu wanajichukia kwa sababu mbali mbali, matendo, maumbo, tabia.................... lakini ukikutana na mtu ambaye either atakuhakikishia kuwa haupo vile unavyojifikiria or akakupenda regardless unaweza ukabadilisha mtazamo wako kwako.
 
upo sahihi kabisa mkuu,
kama umegundua kuna hicho kitu kwa mwenzio ni bora ukamsaidia kuliko kuingia mitini kama ulivyofanya. imagine ungekuwa ni wewe then mwenzio akapotea utajisikiaje?
hii ina-apply hata kwa urafiki wa kawaida tu ambao hauhusiani na mapenzi............. utakutana na mtu ambaye kiukweli amekata tamaa, na hajipendi tena, huyo ni wa kumsaidia sana ili aweze kujipenda na maisha yaendelee
 
Hii kazi inawashinda wengi aisee
rafiki, I bet na wewe imeshakushinda, ha haaaaaaaaaa.
sishangai sana kulisikia hili kwa wakaka, naamini wanapoingia kwa mahusiano wanategemea sana kupendwa sababu ndo kitu muhimu wanachokitafuta kwenye mahusiano, ceteris paribus. sasa ukikutana na mtu ambaye uanze kwanza kumponya ugonjwa wa kujipenda mwenyewe, then aanze kupenda wengine........ (huwezi kujua ataanza kumpenda nani baada ya kujipenda yeye) mpaka ifike zamu yako........ lol!
 

Duh umezungumza kitu wengi hatukukifikiria
wakishapona na kujitambua
chance ipo ya kuja kumpenda mwingine aisee duh..lol
na wewe kazi yako ikawa ni kama dokta tu lol
 
nakumbuka kuna wakati hapa kulikuwa na thread mtu anajihesabia mara ngapi amekuwa approached na wakaka kwa wiki, nikawa najiuliza maana ya hiyo statement sikuipatia jibu sahihi
 
nakumbuka kuna wakati hapa kulikuwa na thread mtu anajihesabia mara ngapi amekuwa approached na wakaka kwa wiki, nikawa najiuliza maana ya hiyo statement sikuipatia jibu sahihi

Na kuna mwingine 'ameolewa kabisa'
but asipotongozwa tongozwa anaugua lol
 
Duh umezungumza kitu wengi hatukukifikiria
wakishapona na kujitambua
chance ipo ya kuja kumpenda mwingine aisee duh..lol
na wewe kazi yako ikawa ni kama dokta tu lol
lakini kama ulifanya kwa mapenzi ya dhati utakuwa na amani kuwa umefanya kitu cha maana, uponyaji........ au unaonaje?
 
lakini kama ulifanya kwa mapenzi ya dhati utakuwa na amani kuwa umefanya kitu cha maana, uponyaji........ au unaonaje?

Hahaha inategemea na mtu
ndo maana tukasema love is a selfish thing hhuko nyuma
 
Na kuna mwingine 'ameolewa kabisa'
but asipotongozwa tongozwa anaugua lol
hilo nalo neno.
kuna kipindi nilikuwa nachukia sana mtu akinitongoza wakati anaona kabisa nina "makufuli" kidoleni. nikagundua kuwa hawayajali sababu hata sisi wavaaji hatuyajali, yamekuwa ni mapambo tu, lol!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…