Kwa hili sipo ukurasa mmoja na wewe. Kikwete ni lazima aendelee, sababu ninazo.
1. Miaka 5 ya mwanzo ilikuwa ya kulipa fadhila kwa waliomuweka madarakani na hilo ameisha lifanya. Miaka mitano ya mwisho itakuwa ya kutengeneza legacy, hivyo ninaimani uswahiba utaisha
2. Miaka 5 ya mwanzo ilikuwa ni learning curve na sasa amefahamu vizuri kuwa urais si kuendeleza urafiki bali ni kufuata taratibu.
3. Miaka 5 ya mwanzo ilikuwa ya kujijenga ili jamaa wasimtose katika miaka 5 ya mwisho, hivyo ninatumaini kuwa miaka 5 ya mwisho itakuwa ni miaka ya kikwete mwenyewe si ya wanamtandao, kwani fadhila kishawalipa. Hivyo atakuwa serious zaidi katika kudeliver
4. Nina hakika ufisadi hautaendelea katika miaka 5 ya mwisho kwani hataangaliwa mtu sura, Kumbuka hotuba yake ya ufunguzi wa bunge?
Kwa kuwa raisi ni lazima atoke CCM kwa vyovyote (Tume ya uchaguzi ni yao, Polisi wao) hivyo lazima wajitangaze ni washindi hata wasipopigiwa kura. Kumbuka kuwa kwenye kila kituo kimoja cha kura cha halali kuna vituo "feki viwili" kwa kauli mbiu yao kuwa 80% ya watanzania wapo rural areas na huko CCM inapendwa kweli kweli. Hivyo basi ni lazima Kikwete aendelee, Kampeni zetu ziwe za kumshawishi huyu bwana sasa umefika wakati avae sura yake halisi yaani sura ya "J M Kikwete" aliyefunga akaunti ya Kighoma Malima yenye mabilioni bila woga. Tukiweza kumrudisha Kikwete huyu nina imani mafisadi watakuwa hawana nafasi. Kikwete ambaye washauri wake hawatakuwa kina Kingunge, Makamba, Lowassa, RO.
Vinginevyo hizi kempeni zitaishia kwenye mtandao na mafisadi wataona kuwa njia pekee ni kumueleza kuwa "Either you are with us or you are alone, because the other side doesn't like you either"