Ni kweli una hoja, umefikiria nje ya box, hiyo inaitwa hypothesis unachopaswa ni kuiongezea nyama, kuipa hoja zilizoshiba. Kama huna kitu cha kufanya haupotezi muda, ila muda unaenda tu bila ya wewe kufanya kitu. Ni sahii kabisa watu wasio na kitu cha kufanya muda kwao ni very irrelevant, hawaufuati na hawashughuliki nao. Kimsingi wako huru sana na wanafurahia maisha bila yakuwa na fedha (hawazezi kupata fedha bila ya kufanya kazi na kufuata muda labda u-bet). Mara nyingine najiuliza maswali mengi sana, huwa nahisi maisha ya kutafuta fedha yametuweka utumwani, tumekua watumwa na maisha yetu wenyewe. Hii nakubaliana na Dalai Lama kama ninavyo quote hapa chini:
“Man. Because he sacrifices his health in order to make money.
Then he sacrifices money to recuperate his health.
And then he is so anxious about the future that he does not enjoy the present;
the result being that he does not live in the present or the future;
he lives as if he is never going to die, and then dies having never really lived.”