Kwa kufuata kanuni za Einstein za "Relativity", hakuna muda halisi na muda unategemeana na mwendokasi pamoja na nguvu za uvutano.
Kwa maana hiyo, kadiri unavyozidi kuongeza kasi, ndivyo unavyozidi kuupunguza upitaji wa muda.
Kwa sayansi za Einstein, ukiweza kufikia mwendokasi wa mwanga (299 792 458 m / s) unaweza kuusimamisha muda.
Kinadharia, ukiweza kupita mwendokasi wa mwanga, utaanza kurudi nyuma katika muda na kuweza kujiona wewe mwenyewe unavyokuja.
Nasema kinadharia kwa sababu katika uhalisi, kitu chochote chenye uzito, hata mdogo vipi, hakiwezi kufikia mwendokasi wa mwanga, kwa sababu kila kinavyozidi kukaribia mwendokasi wa mwanga ndivyo uzito wake unavyozidi kukaribia infinity, na kinadharia kitu chochote chenye uzito kikifikia mwendokasi wa mwanga kitakuwa na uzito usio na mwisho.
Kifupi, time travel (kurudi nyuma) kinadharia inawezekana. In fact kila siku ukipanda gari na kwenda mwendo kasi unapunguza kasi ya muda kupita. Kinadaharia, ukiwa umezaliwa na pacha wako hapa duniani, unaweza kumuacha hapa duniani na wewe ukapanda chombo kinachoenda kasi sana kwenda kwenye nyota za mbali, ukirudi, kwa sababu muda utakuwa unapita kwa polepole zaidi kwenye chombo kinachoenda kwa kasi (time dilation) unaweza kukuta pacha wako kazeeka ana mvi wakati wewe bado kijana.
For more on Relativistic time dilation and object contraction see
Chapter 28 - ROL
The time dilation wiki is at
Time dilation - Wikipedia, the free encyclopedia