mkubwa tulifundishwa darasani ya kwamba kuna wa missionary walikuja afrika kueneza neno la MUNGU kwa kila mtu ila je unajua ya kwamba afrika ilikuwa tayari ina mwamini MUNGU na walikuwa na dini zao tayari ila sasa mzungu alichofanya ni anahubiri na kuwapa maneno yatakayo lainisha mioyo yao na kuanza kuwa wakarimu kufanya kila kitu cha mzungu maana waliona wakitumia force ya kupigana kila siku italeta vifo kwao na kwetu mwishoe na kuleta hamasa kwenye jamii na hii ilikuja baada ya waafrika kusafishwa kila kitu kwenye bongo zetu (Brain washed)
Naomba nisieleweke kama naandika kukejeri, kudharau au namna nyingine ya kutoheshimu.
Tatizo kubwa ninaloliona ni ELIMU na kisha, UELEWA. Hii inatokana na mambo mawili makuu: moja, Wafrika hatutaki KUJIFUNZA, pili Wafrika hatufanyi UTAFITI.
Wafrika hatujifunzi, wala hatutaki kujifunza. Maisha tunayoishi ni yale yale: babu - baba - mtoto - mjukuu. Ni watu wa kung'ang'ania mambo.
Wafrika hatufanyi utafiti. Huwezi kujua ukweli wa mambo bila kufanya utafiti. Wafrika hatuchunguzi mambo.
Kwa mfano, elimu rasmi tunayosoma mathalani historia na uraia, tumefanya utafiti kujua ukweli wake? Au tunapokea tu?
Kati ya mambo ambayo mimi kwa mtazamo wangu nayaona ni ya HOVYO - BURE ni hii dhana au mawazo kwamba, Afrika - Wafrika tulikuwa/ tuna DINI yetu. Huu ni upumbavu na ni kosa kubwa mno!
Kama tungekuwa tunajua dini ni nini tusingeshikilia ujinga huu.
Labda, tujiulize: dini ya Mwafrika ni ipi? Mwanzilishi wake ni nani? Na kwa vipi dini ya Mwafrika inatofautiana na dini ya Kikristo?
Jiulize pia, kwa mfano, Yesu ni dhahiri hakuwa Mzungu. Lakini kwanini mataifa ya Ulaya na Marekani yanamfuata na kumshikilia yeye?
Lakini pia, kama ni kuhusu dini za asili, unafikiri Wazungu - Ulaya, Amerika, hawakuwa na dini za asili kama ilivyo kwa Wafrika - Afrika?
Kando na hapo, kuna vitu hivi: SERIKALI na KANISA - DINI.
Kanisa ndiyo linajua maisha ya mwanadamu: mwanzo wake na hatima yake, wapi anaelekea. Hii maana yake ni kwamba, mfumo wa maisha ya mwanadamu: maadili, ndoa, uzazi na uchumi unatengenezwa na Kanisa - dini, huku serikali wajibu wake ni kusimamia tu - ulinzi.
Kama Wafrika hatutabadilika na kuacha uongo hakuna kitu maadili, maarifa, teknolojia uchumi au maendeleo kitakuwepo.
Tukubali kujifunza, tufanye utafiti kwenye mambo ya msingi: dini, elimu na historia tutapata ukweli. Hapo ndiyo tutajikomboa.
Mawazo ya kufikiri na kuona jamii nyingine isiyo Mwafrika kama ndiyo waharibifu, ni makosa makubwa sana.
Hawa wazungu ni jamii ya dunia. Wafrika pia wanaishi duniani - ni jamii ile ile. Kwa vipi utakwepa ukweli huu, kwamba Wazungu si sehemu ya jamii yetu wakati tunaishi dunia moja?
Katika kuishi jambo la kuzingatia ni kujua jamii yako. Usipozingatia na kuelewa jamii yako hakuna utakachofanya katika maisha: maadili na elimu, maendeleo na uchumi.
Ni vema tusipotoshe, hata kama baadhi yatu tunanufaika na mfumo huu ovu. Madhara yake ni makubwa - muda utafika hatutaweza kuyalipa.