Hii iko kiimani zaidi kuliko intelligence naomba nijibu maswali yako haya kwenye mada itakayojitegemea... Nitafanya hivyo kwa ajili yako lakini nitaomba pia usaidizi wa
Nundu_Tanzania
[/
Ninakushukru ndugu Mshana.
Kuhusu maswali ya ndugu Kenzy, "...Mungu na sifa zake zote tunafaida nae gani katika haya maisha ikiwa katuumba tuishi na tufe...". Nafafanua kama ifuatavyo:
Ukitazama, kati ya viumbe vyote, mwanadamu anajitokeza kiumbe bora kushinda vingine vilivyoumbwa vinavyoonekana.
Jicho bila mwanga linabaki jina tu. Mungu ametushirikisha kwa namna ya pekee uungu wake kushinda viumbe vyote vinavyoonekana.
Akili tuliyonayo ni sehemu ndogo sana ya uungu wa Mungu kwetu.
Mwili : nyama na damu, siyo chochote, bila ya roho. Pasipo roho mwili hauwezi kufanya kazi.
Kama tunaishi, basi ni kwa sababu ya roho. Kama ilivyo kwa jahazi haliwezi kusafiri majini, bila ya mtu kuliendesha. Vivyo hivyo, mwili hauwezi kufanyakazi (kusafiri ulimwenguni), bila roho.
Aidha, kifo siyo hasara. Mwanadamu ameumbwa kufa. Lakini kifo hakina maana kwamba, ndiyo mwisho wa maisha isipokuwa ni mwisho wa safari yake hapa duniani.
Kama alivyo mwanadamu anasafiri, yumo njiani kuelekea utimilifu wake, Mungu. Vivyo hivyo dunia nayo imo njiani kuelekea utimilifu wake, inasafiri itafikia ukomo wake, Mungu.
Nafasi na muda wa mwanadamu, nafasi na muda wa dunia. Vyote vinaelekea nguvu ile ile hai, Mungu.
Kuhusu Mungu anafaida gani na mwanadamu kwenda motoni au peponi.
Ulishajiuliza: Je, wazazi wanafaidikaje na mtoto afanyae maovu au mema? Au jiulize hivi: Je, mtu kwa kutenda mema na mwingine kwa kutenda maovu nani anafaidika?
Kuhusu hili swali lako, jibu lake ni kwamba, hilo ni suala la maadili.