Timu ambazo hazitashiriki hatua ya awali ligi ya mabingwa. Simba miongoni mwa timu 10 zilizoorodheshwa

Mkuu, hebu kuwa mkubwa kuliko hao unaowatuhumu.

Kuwaombea mabaya wengine badala ya ku focus kujiimarisha mwenyewe ni small team mentality.
Kwa shabiki wa Simba kuwaombea Yanga watolewe hatua za awali, bado nawewe unakua kwenye hiyohiyo "small team mindset"

Bila kuangalia wao wanaYanga wana_behave vipi, ni lazima sisi kama wanaSimba tujipambanue kwamba kuna ka ushamba fulani hatunako tena. Not anymore.

Kuwaombea hao watu mabaya hasa katika mashindano ya kimatatifa, ni dalili za wazi kwamba ukipata muda, unaweza kwenda Airport kuwapokea wapinzani wa Yanga.

Hizi nafasi nne za nchi tunatakiwa kuzilinda kwa umoja wetu, zimeletwa na mtu mmoja (Simba SC. ) hazipaswi kulindwa na mtu mmoja huyohuyo.

Tukue
 
Mkuu umemaliza. Tatizo kubwa ni kuwa baadhi ya mashabiki wa Simba hawataki kuamini kuwa unaweza kupita upepo mbaya Simba ikashindwa kupata nafasi ya moja kwa moja kushiriki kimataifa kupitia kwenye ligi na FA. Lakini kama taifa lina nafasi nne itawasaidia pia wao kama Yanga walivyofaidika mwaka huu. Sioni sababu ya kuanza kuombeana eti timu fulani itolewe mapema badala yake ni kuunganisha nguvu kama taifa ili hizi nafasi nne ziwe za kudumu. Mabaya tuombeane humu humu kwenye ligi ya ndani basi.

Kitendo cha kuwaombea mabaya Yanga kwa sababu tu eti waliiombea Simba mabaya tayari kinawafanya mashabiki wa Simba wasiwe tofauti na baadhi ya mashabiki wa hovyo wa Yanga. Lakini niwakumbushe tu mashabiki wa Simba kuwa ustaarabu wao wa kutokwenda kukesha uwanja wa ndege eti kuwapokea wachezaji wapya waliosajiliwa na kuanza kuwabeba na kuwazungusha Dar nzima kwenye magari ya wazi hawaoni kuwa kimewafundisha ustaarabu mashabiki wa Yanga. Na hata mwishoni mwa CL wale baadhi ya mashabiki wa hovyo waliokuwa wanapokea timu pinzani na Simba waliyeyuka kama barafu pale uwanja wa ndege.

Mungu libariki soka la Tanzania.
 
Br, Tuwe wa kweli . hivi wewe utafuarahi Yanga achukue ubingwa wa Africa kabla ya simba, Kwenye mpira uwezi kumuombea mshindani wako afanikiwe. Yaani eti man u wamuombee Liverpool achukue ubingwa? Zamaleki amuombee Al Ahly achukue ubingwa? Akipambana akachukua tunampongeza. Uzalendo Upo. Timu ya Taifa, uku kwenye vilabu kila timu na malengo yake
 
If wishes were horses....

Hakuna aliyesema wewe shabiki wa Simba uiombee Yanga ichukue Ubingwa wa Afrika.

Kama unaamini maombi yanasaidia, basi iombee timu yako (Simba) ichukue ubingwa wa Afrika.

Tunachokishangaa na kukipinga ni pale ambapo shabiki wa Simba, unaiombea Yanga iishie raundi za awali.
Hili likitokea lina madhara sio kwa Yanga peke yake, linahatarisha kuendelea kuwepo kwa nafasi nne za nchi.

Sitaki kuamini kwamba kuna mtu Usimba umemkolea kiasi kwamba anaona nchi kuendelea kuwa na nafasi nne si mali kitu.

Mtu wa hivi anakua hana tofauti sana kiitikadi na yule anayeenda uwanja wa ndege kuipokea timu ya nje.

Mwisho wa siku uhuru wa nini na nani wa kumuombea unabaki kuwa wako.

Unaweza kuiombea Yanga ijifie, au Al Ahly ipotee kwenye ramani ya soka, au Azam ishuke daraja, n.k

Fanya yale unayoona yana mashiko, lakini kumbuka kuwa reasonable.
 
Moja ya vitu kwenye mpira vinavyofanya tuendelee kushindana ni huku kuzodoana. Yanga haiwezi kutofanya vizuri kwa sababu shabiki wa simba anaomba iishie priminary round. Ubora wao ndio utawafanya wafike mbali. Point ni kwamba tunamcheka na kusema yanga ishie round ya kwanza ndio iwape Yanga hasira na kua bora. Shabiki wa simba hawezi kuiombea mazuri Yanga ndivyo na kwa Yanga vivyo hivyo
 
Kumbe timu ikishinda kombe la klabu bingwa ulaya jezi zao zinawekwa nyota.
 
Habari hii ingemkuta Manara akiwa msemaji pasingetosha mjini hapa ... Sema ndo hivyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…