Timu France mpo wapi amkeni amkeni

United ya Ferguson

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2021
Posts
3,132
Reaction score
6,353
Mashabiki wa timu ya taifa ya France mbona mmejikausha kana kwamba sio mabigwa watetezi wa kombe la Dunia amkeni mliko jificha tusiende mbali sana France ndio bigwa mtetezi wa kombe hili kwahyo lazima tutembee kifua mbele sjataka

kuandika rekodi za France kweny kombe la Dunia nitawavuruga watu vichwa labda Brazil wataupa msaada wa rekodi zetu maana tuliwapusa kweny fainali ya 98 tukawapasua na kweny mechi ya Robo fainali mwaka 2006 pale Germany mzee mzima zizoo alimtia kidali Ronadhniho gaucho

France tupo kundi D tukiwa pamoja na timu za Australia, Denmark pamoja na Tunisia kutoka Africa
Katika timu ambayo tumepata kundi kidogo lenye unafuu ukilinganisha na wengine ni France

Kweny kundi letu mpizani mkubwa namuona ni Denmark na Australia hawa ni wapinzani ambao tulikua nao kweny kundi moja mwaka 2018
Kilichobadilika hapa ni Tunisia pekee

Kuhusu majeruhi inajulikana chirspoher nkuku ndio kapata majerah ila nafasi yake imechukuliwa na Marcus Thuram mtoto wa nyota wa zamani wa timu ya taifa ya France
Ratiba ya mechi za France ipo kama ivi

1 22/11/2022
France vs Australia 7.00 pm Kwa saa za Africa mashariki mechi itapigwa kweny uwanja wa Al janoub stadium

2 26/11/2022
France vs Denmark 16.00 pm Kwa saa za Africa mashariki mechi itapigwa kweny uwanja wa 974

3 30/11/2022
Tunisia vs France 3.00 pm Kwa saa za Africa mashariki mechi itapigwa kweny uwanja wa education city hii ndio itakua mechi ya mwisho ya makundi ya France
 
Mbona tupo tumevimba mashavu, tangia tumebeba world cup mpaka leo hii tumenenepeana mno kwakweli.
 
Safu ya ushambuliaji ipo vizuri ila midfields wananipa khofu.
 
majeruhi tulio nao wafaransa ni watu muhimu sana nina was was sana kwenye hii WC
 
majeruhi tulio nao wafaransa ni watu muhimu sana nina was was sana kwenye hii WC
asee benzema naye out mbona tunashida magoli yamepunguka kabisa Yani Kwa watu wa mbele mwenye uwezo wa kufunga kabaki mbape pekee manaa grizeman kashuka sana sio yule wa siku zote
 
Matheo guondozi yupo timu gani sikuhizi?
 
Ukivuka group stage niite mbwa niko pale nimekaaa .....!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…