Afrika ni Afrika tu,Na wa Afrika ni wa Afrika tu
Timu ya al Ahly inayojiandaa kucheza na yanga desemba 02,2023 imezua gumzo la mwaka kwa kusafiri na mizigo mingi iliyopita kiasi na kuhitaji gari tatu ,Basi moja kubwa la Happy Nation,Coastal moja ,Pamoja na Noah moja lakini bado gari zote hizo hazikutosha
Maafisa wa Al ahly wameonekana wanasubiri gari ya nne nyingine naona hii itakuwa kali ya mwaka
Kumbuka siku ya maandalizi ni moja tu imebaki yaani ni leo tu ,Watu wanabeba mizigo iliyopitiliza mpaka wanakosa nafasi za kukaa wenyewe
Cha kushangaza na kusikitisha ni pale waarabu walipoogopa kupitishia mabegi mlangoni na kuamua kupitishia dirashani,Mwandishi amejitahidi kuwaonyesha mlango wa coastal ambao upo wazi na mkubwa lakini bado akabaki mdomo wazi kwa kinachoendelea kwa waarabu kuogopa kutumia mlango wa coastal na kuamua kupitishia mabegi dirishani
Waarabu wanaogopa mlango wa coastal na hizi ndizo imani za Afrika,Mpira wa Afrika bado una safari ndefu na unaamini katila ulozi na uchawi
Tumezoea Al ahly wanasafiri na majaba , maplastic na mapipa makubwa na kweli wamekuja nayo lakini wamekuja na vituko vya kuwa na mizigo mingi ambayo hata ungeleta fuso isingetosha
Kilichonichekesha na hata kuwashangaza waandishi wa habari ni kitendo cha kuja na masanduku ambayo huwezi kuyasukuma kwa vifaa vya airport bali ni kwa kuyaburuza ambayo waliyapakia kwenye Noah