Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
TEAM YA AL FATAH ONLINE TV WALIOPOTEMBELEA MAKTABA KWA MAHOJIANO
Sijawahi kufanya kipindi cha namna hii na kwa mtindo huu.
Nilimwambia Rashid na wenzake Talib na Juma kuwa Maktaba ina mitaa na ningependa kuwatembeza kuwaonyesha mitaa hiyo.
Nilidhani ni kazi nyepesi.
Waingereza wana msemo, "A walk in the park."
Kama vile kusema kunyoosha miguu.
Nikaanza na kitabu cha kipya cha maisha ya Mohammed Abdulrahman alichoandika baada ya kupumzika kazi Sauti ya Ujerumani.
Salim kafurahi sana.
Kampigia simu Mohammed ananiambia ni mwalimu wake kamfunza mengi katika tasnia ya habari.
Mohammed ndugu yangu mwana Kariakoo mwenzangu kakulia mtaa wa Ukami karibu na Msikiti wa Manyema.
Kitabu chake nimekisoma na kinavutia.
Lakini kubwa kanifunza na kunionyesha vichochoro vya kupita ikiwa na mimi nitataka kuandika kitabu kama yeye.
Hii ilikuwa bashraf.
Tunaingia mtaa wa kwanza.
Nawaonyesha kitabu.
Wala si kitabu.
Fotokopi ya kitabu cha Sheikh Ali Muhsin Barwani, "Conflict and Harmony in Zanzibar," kanipa Ahmed Rashaad Ali mwaka wa 1999.
Tumeongozana mguu kwa mguu kutoka kwake Upanga hadi Mtaa wa Jamhuri Topaz kutoa fotokopi.
Nakala ya kitabu imeingizwa kwa siri.
Jina la Ali Muhsin linatisha sikwambii uwe na kitabu chake.
Leo buku la Khamis Abdulla Ameir linaingia Zanzibar bila tabu na waheshimiwa wanapiga simu Masomo Bookshop wawekewe nakala.
Kijana wa fotokopi ananifahamu.
Tumefanya mengi pamoja ya staili hii.
Zile zilikuwa siku nyingine.
Msondo ngoma akili kichwani mwako.
Haya nayaeleza.
Wasikilizaji wangu wamevutiwa na stori.
Sura zao naziona.
Hawajapata kupitishwa mitaa hii.
Mtaa huu mrefu na Salim namwona hataki tuondoke.
Anataka nimweleza Sheikh Ali Muhsin alivyotoroka Tanzania.
Ni movie ya Spielberg.
Nawaeleza vipi miezi miwili tu baada ya kusoma kitabu cha Ali Muhsin nikajikuta Muscat nazungumza na Sheikh Ali Muhsin.
Mzee Rashaad alinieleza kuwa Ali Muhsin kasoma Qur'an yote nyumbani kwao kasomeshwa na baba yake na shule hadi Makerere alikuwa A Student.
Kwa tabu nikawatoa mtaa huu kuingia mtaa mwingine na mwingine na mwingine.
Kama si Adhana ya Maghrib...
Natazama nje kiza kimeingia kimetufunika.
Wanasema Maktaba imesheheni stori na mikasa.
Nawaeleza enzi za kale na majarida ya kila mwezi kutoka London.
New African na Africa Events.
Wahariri Anver Versi na Mohamed Mlamali Adam.
Hawa wote tunafahamiana na Ahmed Rajab ndiye kanifikisha kwao.
Wakanipenda na wakawa wanachapa makala zangu.
Mlamali anajua kucheza na Kiingereza na anajua kuchagua maneno.
Anaandika taazia hujui kama ni taazia au ni "satire" ndani ya taazia.
Unasoma msiba lakini unacheka.
Wamefika kwangu.
Upele umempata mkunaji.
Leo Maktaba ilikuwa imetembelewa na magwiji kutoka Zanzibar.