Timu ya Biashara United imeshambuliwa vibaya sana. Viongozi wao wawili hawajulikani walipo

Timu ya Biashara United imeshambuliwa vibaya sana. Viongozi wao wawili hawajulikani walipo

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Biashara United Mara wamefika mkoani Tabora na kupokelewa kwa kipigo asubuhi hii wakati wanaenda kwenye pre match Meeting.

Technical director Omary Madenge ameshambuliwa sana yupo kwenye hali mbaya lakini pia amenyang’anywa baadhi vitu alivyokuwa navyo.

Pamoja na hayo viongozi wawili wa Biashara United Mara hawajulikani walipo, wamechukuliwa na kupelekwa kusikojulikana.

Kwasasa gari iliyovamiwa na kushambuliwa ipo Polisi lakini hakuna ushirikiano wowote wa Polisi. Taarifa zinaonesha kuwa hakuna ulinzi wowote ambao Biashara United watapewa.

Screenshot 2024-06-16 115612.png
 
Huu ni UPUMBAVU inabidi biashara waindiakie TFF barua ya kuomba kuahirishwa mechi ikachezwe moja mwingine (neutral ground)
Kwa ground zipi, za kushambuliwa tu..?
Kama wame stage wenyewe hilo shambulizi..?
Sheria zipo wazi, sababu za nje ya uwanja haziwezi kufanya match iwe postponed, unless uwanja uwake moto labda au mashabiki waingie na mapanga which is impossible.
 
Sheria ichukue mkondo wake hizi hooliganism hazifai na inabidi zikemewe na kuzimwa pindi zinapoanza kuchipua...
watu wana wachezaji wao na agency imeweka pesa. hili ni trailer tu more is coming
 
Hili nililiona tangu mapema biashara wanahitaji kuwa na utulivu na Kutumia mbinu za kivita kuvuka vikwazo vya Leo
 
Back
Top Bottom