Tarehe 28 mwezi Mei, timu ya madaktari ya kikosi cha 25 cha walinda amani wa China nchini Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC) walitembelea Kituo cha kulelea Watoto yatima cha shirika la kibinadamu SOS huko Bukavu wakati Siku ya Kimataifa ya Watoto ikikaribia.
Waliwazawaida watoto wa pale vifaa mbalimbali vya masomo na zawadi nyingine zenye umaalum wa kichina, wakitumaini watoto hao watajifunza kwa bidii na kuwa na furaha. Pia waliwapa watoto hao vifaa vingi vya kujikinga na maradhi vikiwemo vitakasa mikono na barakoa, na kuwafundisha namna sahihi ya kunawa mikono ili kujikinga na bakteria, wakihamasisha watoto hao kudumisha tabia nzuri za afya.
Mfanyakazi mmoja wa kituo hicho alisema, siku zote timu ya madaktari ya kikosi cha kulinda amani cha China ilifuatilia hali ya watoto, na baadhi ya wakati watoto wanakwenda hospitali ya timu hiyo kupata matibabu.
Tangu mwaka 2005, timu ya madaktari wa kikosi cha kulinda amani cha China ilianza kutoa misaada mbalimbali kwa kituo hicho.