Timu ya taifa ya Chad yajitoa michuano ya kufuzu kombe la mataifa ya Afrika (AFCON 2017)

uamuzi huu wa chad unainufaisha misri zaidi!
 
Dah! Fitna za Misri zimetutia kidole.
Ndo bye bye tena.
 
Ufafanuzi tafadhari hii maana yake nini,ina maana kule Gabon timu zitakazoshiliki ni pungufu ?? ( kwa mujibu wa wadau hapo juu wanasema eti sasa kundi letu litatoa timu 1 na si 2 ) ina maana zile nafasi 2 inazibwa vipi ili Gabon zisiende timu pungufu ???
 
Inahusu best loser.Hivyo kundi G haliwezi kutoa best loser kwasababu team zipo tatu tu.
 
Kuna mwaka fulani moza.bique alipata best looser akiwa na point chache wenye point nyingi wakabaki.kuna vitu vingi wanaviangalia siyo idadi ya point tu.
 


Timu ya Taifa ya Chad ‘Les Sao’ imejiondoa katika michuano ya kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika (AFCON) itakayofanyika mwaka 2017 nchini Gabon.

Taarifa ya kujitoa kwa Chad imetolewa na Shirikisho la Mpira wa miguu barani Afrika (CAF) leo baada ya Les Sao kuandika barua ya kujitoka katika mashindano hayo ikiwa katika kundi G pamoja na timu za Tanzania, Nigeria na Misri.

Chad ilitarajiwa kucheza kesho Jumatatu dhidi ya Tanzania katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, ikiwa ni mchezo wa marudiano wa kundi G baada ya kucheza mchezo wa awali jijini N’Djamena katika ya wiki.

Katika mchezo wa awali uliochezwa uwanja wa Idriss Mahamat Ouya, Taifa Stars iliibuka na ushindi wa bao 1- 0, bao lililofungwa na nahodha Mbwana Samatta dakika ya 30 ya mchezo.

Kufuatia kujitoa kwa Chad, matokeo ya michezo yote iliyoihusisha timu hiyo yanafutwa, na msimamo wa kundi G kwa sasa unaongozwa na Misri yenye pointi 4, Nigeria pointi 2 na Tanzania pointi 1.


Chanzo: Karibunjombe

============

UPDATE

TFF yathibitisha kujitoa kwa CHAD AFCON
 
Kwanza nimeumia sana kwa Timu ya chad kujitoa katika mashindano kwani chad ingetupa point 6 ambazo zingetusaidia kuweza kushika nafasi ya kwanza au pili lakini baada ya chad kujitoa tumaini limefifia
ushauri kwa TFF
-Caf wachunguze kujitoa kwa chad maana naona ni kama njia ya kuihujumu TANZANIA isipite ukipiga mahesabu utagundua chad angeisaidia TANZANIA kupita kwa iyo TFF iiandikie CAF ili chad wachunguzwe
 
mi sioni sababu ya watu kukosa amani na hiki kitendo cha Chad....nafasi ya kupita bado ipo, cha msingi ni kutoa vipigo kwa wapinzani wetu; na kama 2kishindwa kufanya hivyo basi kweli hatustahili kupita...
 
Tupe msimo wa kundi, ukoje? Na kama wamejitoa si hata zile poti za timu nyingine zilizocheza na Chad nazo si zina potezwa yaani matokeo yote ya timu zilizo cheza na Chad yanafutwa....!? Hivyo kama tulishindwa kuvuna kwa hizo timu zilizobaki tuache visingizio.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…