Melubo Letema
JF-Expert Member
- Apr 1, 2020
- 416
- 414
Shirikisho la Riadha Tz (RT) tunapenda kuwajulisha wanachama, waalimu, na wadau mbalimbali kuwa wanariadha wetu wawakilishi wa mashindano ya Dunia ya Mbio za nyika wameshindwa kusafiri kutokana na Changamoto ya kupatikana kwa Visa.
Wanariadha hao ambao walitarajiwa kuondoka jana tarehe 27/03/2024, ililazimika kusogeza mbele safari yao hadi siku ya leo tarehe 28/03/2024 baada ya kuchelewa kupata visa kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu.
Changamoto hii ya visa umewakumba pia baadhi ya nchi majirani kama Kenya, Ethiopia, Uganda, nk
Maombi ya Visa yalifanyika tangu tarehe 08/03/2024 kupitia ubalozi wa Serbia uliopo Nairobi Kenya.
Lakini mpaka kufikia tarehe 27/03/2024 ni wachezaji watano tu waliokua wamepata visa kati ya wanariadha Tisa( 9)
Hata hivyo wanariadha waliopata visa walishindwa kusafiri jana kwakua passport zao zilikua zimechelewa kutoka ubalozi Nairobi na zilifika Tanzania kwa kuchelewa hali iliyotulazimu kubadili ticket ili waondoke leo(27/03/2024).
Usiku huu Rais wa RT Silas Isangi ameongoza msafara wa kusindikiza wanariadha hao, lakini ndege waliotarajia kusafiri nayo ya KLM imechelewa kufika uwanja wa ndege wa KIA na hivyo kufanya uwezekano wa wanariadha kufika Serbia kabla ya mashindano kuwa haupo kwa kuwa ndege yao ya kutoka Amsterdam kwenda Serbia inaondoka Amsterdam.
tarehe 29/03/2024 saa nne asubuhi, muda ambao ndege ya kutoka Tanzania kupitia Entebe itakuwa haijafika Amsterdam kwa ajili ya connection ya kwenda Serbia.
Jacob Kiplimo kutoka Uganda, akimalizia mbio na mshindi wa Mbio hizo Kwa dakika 28:08.