Jacobus
JF-Expert Member
- Mar 29, 2011
- 4,703
- 1,724
Nimepitia humu sijaona chochote na pia 'website' ya TFF kimya tena hii haina taarifa ya kitu kinachoitwa CHAN 2021.
Nimetafuta hii kutaka kufahamu kama TFF wameamua chochote kuhusu kocha wa timu hiyo kutokana na matokeo mabaya tokea kuteuliwa kwa kocha huyo licha ya haya ya CHAN 2021.
Watupe neno basi ili sie wananchi tuelewe kinachoendelea kwenye timu hii ya Taifa.
Nakumbuka kwenye mashindano ya AFCON mpaka serikali kupitia kwa waziri wa michezo wakati huo mhe Mwakyembe alisema kocha Amunike aendelee kuifundisha timu hiyo, lakini ilipotolewa mzunguko wa mwanzo na kurejea nyumbani TFF haikuchukua muda ikamtimua.
Sasa huyu mie sijasikia chochote na jana ndo ilikuwa nusu fainali ya CHAN kwa timu za Morocco na Mali kuingia fainali, najiuliza kama timu yetu imeisharejea nini kinafuata au kama bado ipo huko inafanya nini mpaka sasa?