Binafsi nilifuatilia mchezo baina ya Tanzania na Guinea ya Ikweta. Niseme kutoka rohoni hatuna timu ya Taifa. Mchezo waliocheza siku ile ni mbovu sana. Naishauri TFF kwanza tujitoe kwenye michezo ya Kimataifa. Tusuke timu kwanza ndipo turudi kwenye mashindano. Rais wa TFF ajiuzulu na tangu ashike wadhifa huo hakuna matokeo chanya Timu ya Taifa imepata. Ni bora hata tungepeleka timu ya Ihefu ikacheza nao tungepata matokeo chanya. Inauma sana.