Timu ya Taifa ya Ngumi za Wanawake yaagwa Rasmi

Timu ya Taifa ya Ngumi za Wanawake yaagwa Rasmi

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,278
Reaction score
797
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ameiaga rasmi timu ya ngumi ya Wanawake ya Tanzania inayokwenda kushiriki mashindano ya Ubingwa wa Dunia kwa upande wa Wanawake yatakayofanyika katika mji wa New Delhi nchini India Machi 15 hadi 26 mwaka huu.

Akiiaga timu hiyo leo jijini Dar es Salaam, Waziri Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ameeleza kuwa Tanzania imekuwa ikipata mafanikio katika mashindano mbalimbali ya Kimataifa akisisitiza kuwa mafanikio hayo yanapaswa kuwa endelevu huku akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha na kuimarisha Sekta ya michezo nchini.

“Kwa namna ya pekee natumia fursa hii kumshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania kwa kuendelea kuboresha na kuimarisha Sekta ya Michezo hapa nchini, hii ni Sekta muhimu inayogusa maisha ya Watanzania wengi bila kujali umri wao” Ameeleza Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana.

Ameongeza kuwa Serikali inathamini na kutambua mchango wa Sekta ya michezo nchini ndio maana imefungua milango kwa Sekta Binafsi na kukaribisha wawekezaji kwenye eneo la miundombinu, uibuaji na uendelezaji wa vipaji kwa vijana ili kuzalisha vipaji na watalaam wa michezo hapa nchini.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Saidi Yakubu amesema ushiriki wa Serikali katika kufanikisha safari na ushindi wa timu hiyo ni mkubwa kwa kuzingatia kuwa umekua ukiiwezezesha Tanzania kufanya vizuri kwenye mashindano ya Kimataifa.

“Tunajivunia kuwa na mchezo huu kwa sababu mwaka 2022 ulitutoa kimasomaso na kulifanya jina la nchi yetu litambulike. Natumaini wawakilishi wetu hawa watakwenda kupambana na kutuletea ushindi, Nawaomba Watanzania wanaoishi nchini India wajitokeze kwa wingi kuwashangilia vijana wetu” Amesisitiza.

Katika mashindano hayo Tanzania inawakilishwa na Rahma Joseph Maganga na Beatrice Ambrose Nyambenga huku zawadi zitakazotolewa kwa washindi katika mashindano hayo ni Medali ya Dhababu, Medali ya Fedha na Medali ya Shaba.View attachment 2547801View attachment 2547800View attachment 2547803View attachment 2547802View attachment 2547804View attachment 2547806
IMG-20230312-WA0063.jpg
 
Back
Top Bottom