Timu ya Taifa ya Riadha Olimpiki yatua Dar, kesho kupaa Paris, Ufaransa

Melubo Letema

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2020
Posts
416
Reaction score
414
870e6207-0bfa-4b7e-a578-fb34554e753b.jpeg

Pichani : Kutoka kushoto ni Magdalena Shauri, Gabriel Gerald Geay , Jackline Sakilu na mwisho ni Nahodha Alphonce Felix Simbu.

TIMU ya Taifa ya Riadha itakayoiwakilisha Tanzania katika michezo ya Olimpiki Paris 2024, imewasili jijini Dar es Salaam leo Agosti 6 ikitokea kambini jijini Arusha.

Timu hiyo inayoundwa na wachezaji wanne na kocha mmoja, iliwasili majira ya saa kumi jioni kwa ndege, ikitokea jijini Arusha ilikokuwa ikijifua kwa takribani mwezi mmoja chini ya udhamini wa CRDB Foundation.

Kikosi hicho kimefikia hotel ya Blue Sapphire iliyoko Vingunguti, ambapo watapumzika na kesho Agosti 7 alfajiri kitakwea pipa kwenda Paris kutupa karata ya pekee ya Tanzania iliyobaki katika michezo hiyo.

Akizungumza baada ya kuwasili Dar, Kocha wa kikosi hicho, Anthony Mwingereza, amesema kambi ilikuwa nzuri na mazoezi yamekwenda vema, kilichobaki ni Watanzania kuwaombea dua warejee na medali.

Nahodha wa kikosi hicho, Alphonce Simbu, amesema wanakwenda kupambana na kilichobaki ni sala za Watanzania tu.

Timu hiyo inaundwa na Simbu, Gabriel Geay, Jackline Sakilu na Magdalena Shauri, ambao wote watashiriki katika mbio ndefu ya kilomita 42.2 yaani Marathon.

Soma Pia: Watanzania 7 kupeperusha Bendera ya Tanzania katika Olimpiki 2024 huko Paris
 
View attachment 3063337

Wakaze hadi north korea ana medali aisee
 
Watuambie watashiriki lini sasa tuangalie maana michezo ni mingi naangalia kila siku sioni nchi yetu.
Cheza na hizi tarehe

kweli mkuu, nimekosea,

tunakimbia agosti 10 Men Marathon tunawkimbiaji wawili muda kuanzia saa 3 asubuhi.

tunakimbia tena agosti 11 Women Marathon wakimbiaji wawili muda kuanzia saa 3 asubuhi

Ratiba. ni official website ya olympics
 
View attachment 3063337
Pichani : Kutoka kushoto ni Magdalena Shauri, Gabriel Gerald Geay , Jackline Sakilu na mwisho ni Nahodha Alphonce Felix Simbu.

TIMU ya Taifa ya Riadha itakayoiwakilisha Tanzania katika michezo ya Olimpiki Paris 2024, imewasili jijini Dar es Salaam leo Agosti 6 ikitokea kambini jijini Arusha.

Timu hiyo inayoundwa na wachezaji wanne na kocha mmoja, iliwasili majira ya saa kumi jioni kwa ndege, ikitokea jijini Arusha ilikokuwa ikijifua kwa takribani mwezi mmoja chini ya udhamini wa CRDB Foundation.

Kikosi hicho kimefikia hotel ya Blue Sapphire iliyoko Vingunguti, ambapo watapumzika na kesho Agosti 7 alfajiri kitakwea pipa kwenda Paris kutupa karata ya pekee ya Tanzania iliyobaki katika michezo hiyo.

Akizungumza baada ya kuwasili Dar, Kocha wa kikosi hicho, Anthony Mwingereza, amesema kambi ilikuwa nzuri na mazoezi yamekwenda vema, kilichobaki ni Watanzania kuwaombea dua warejee na medali.

Nahodha wa kikosi hicho, Alphonce Simbu, amesema wanakwenda kupambana na kilichobaki ni sala za Watanzania tu.

Timu hiyo inaundwa na Simbu, Gabriel Geay, Jackline Sakilu na Magdalena Shauri, ambao wote watashiriki katika mbio ndefu ya kilomita 42.2 yaani Marathon.

Soma Pia: Watanzania 7 kupeperusha Bendera ya Tanzania katika Olimpiki 2024 huko Paris
Ikawe kheri kwao
 
Kwa nini wamewekwa kwenye hoteli za vingunguti??
Wanaodhamini ndio wameamua kuwaweka huko Vingunguti.
Upande wa pili, huko vingunguti hakuna hoteli nzuri?
Kama Msasani, Masaki, Osterbay, Mbezi beach napo pia kuna hoteli za ovyo ovyo, hata wangekaa huko kunaweza kuwa ajabu.

Kwangu mimi, wanamichezo wanaojiandaa na mashindano (hususani wanariadha) hawapaswi kukaa kwenye mahoteli, sehemu nzuri na bora ni kukaa kwenye hosteli zenye viwanja vya michezo. Mfano ni kule Chamazi Azam Complex, Kigamboni Avic town, Karume kwenye hosteli za TFF?, Makongo sekondari, Jitegemee sekondari nk.
 
Back
Top Bottom