Timu ya Taifa ya Uingereza iheshimiwe

Timu ya Taifa ya Uingereza iheshimiwe

GenuineMan

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2017
Posts
6,260
Reaction score
14,470
Nimeona kuna kasumba ya watu kuidharau timu hii, imefikia wakati wengine wameanza kuita "Kichwa cha mwendawazimu" na majina mengine ya hovyo.

Kwa msiyojua Uingereza ni kati ya mataifa nane yaliyowahi kushinda Kombe la Dunia.
Yaani toka kombe hili linaanza mwaka 1930, mpaka leo 2022 ni mataifa nane tuu yamewahi kushinda kombe hili na Uingereza ni mmoja wapo.

Mataifa makubwa kisoka kama Uholanzi, Ureno na Ubeligiji, hili kombe huwa wanalikodolea macho tuu.

Uhispania wenyewe wameshinda kombe hili mara moja tuu sawa na Uingereza.
Ufaransa, Argentina na Uruguay mara mbili kila mmoja.
Italia na Ujerumani mara nne kila mmoja.
Brazil ndiye kinara wa kutwaa kombe hili mara tano.

Ukija kwenye 'ranking' Uingereza kwa sasa wapo tano bora.
Pia walifika Nusu Fainali ya Kombe la Dunia 2018 na ni Mshindi wa Pili wa Euro 2020.
 
England licha yakua wanawachezaji Nyota lakini kwasasa Wana timu. Watafika mbali.
 
England nchi yao kuongoza kwa kuwa na wachezaji wa kigeni wengi sana inachangia mno kuathiri ubora wa timu yao ya taifa (The Three Lions).
 
umeandika Kama vile wachezaji wanaounda timu ni walewale walioshinda kombe la dunia kipindi hicho au waheshimiwe kwa kua tayari wamewahi kuchukua ndoo
 
ENGLAND..THE THREE LION'S(IT`S COMING HOME)

Mkuu mzabzab huwa unanikataa sana,subiri dawa yako
 
Mm ni England, France, Portugal na Grman hapa lzm nipate bingwa
 
Uko sahihi kabisa. Ni uingereza aliemwondosha ujeruman kwenye uero iliyopita kwa kipigo cha 2-0
 
Back
Top Bottom