GenuineMan
JF-Expert Member
- Jun 13, 2017
- 6,260
- 14,470
Nimeona kuna kasumba ya watu kuidharau timu hii, imefikia wakati wengine wameanza kuita "Kichwa cha mwendawazimu" na majina mengine ya hovyo.
Kwa msiyojua Uingereza ni kati ya mataifa nane yaliyowahi kushinda Kombe la Dunia.
Yaani toka kombe hili linaanza mwaka 1930, mpaka leo 2022 ni mataifa nane tuu yamewahi kushinda kombe hili na Uingereza ni mmoja wapo.
Mataifa makubwa kisoka kama Uholanzi, Ureno na Ubeligiji, hili kombe huwa wanalikodolea macho tuu.
Uhispania wenyewe wameshinda kombe hili mara moja tuu sawa na Uingereza.
Ufaransa, Argentina na Uruguay mara mbili kila mmoja.
Italia na Ujerumani mara nne kila mmoja.
Brazil ndiye kinara wa kutwaa kombe hili mara tano.
Ukija kwenye 'ranking' Uingereza kwa sasa wapo tano bora.
Pia walifika Nusu Fainali ya Kombe la Dunia 2018 na ni Mshindi wa Pili wa Euro 2020.