Timu ya Tanzania ya Watoto waishio katika mazingira magumu yashika nafasi ya pili katika Kombe la Dunia

Timu ya Tanzania ya Watoto waishio katika mazingira magumu yashika nafasi ya pili katika Kombe la Dunia

tatum

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2018
Posts
5,786
Reaction score
4,491
More than 200 street-connected children from across the world have come together in Russia for their own boys and girls international football tournaments, festival of arts and Congress for their rights.

The Street Child World Cup uses the power of football to raise awareness and tackle the widespread stigma faced by street-connected children, inspiring countries, governments and communities to better protect, respect and support street-connected children worldwide.

CHK_3701-1024x683.jpg


Timu ya wasichana wa mtaani ya Tanzania imeingia fainali baada ya kuwafunga Marekani goli 5 kwa 0 na pia kuwafunga timu ya wasichana ya Uingereza goli 2 kwa 1 katika michezo ya robo na nusu fainali.

Na leo wanacheza mchezo wa fainali na timu ya wasichana wa mtaani ya Brazili katika uwanja wa Sapsan jiini Moscow Urusi saa 11:30 am

Tunawaombea heri na fanaka katika mchezo huo
====

Timu ya watoto wa kike wanaoishi katika mazingira magumu kutoka nchini Tanzania, imefungwa kwa mbinde goli 1-0 na timu ya Brazil katika fainali ya Kombe la Dunia( Street Children World Cup)
Kwa matokeo haya timu hiyo imeshika nafasi ya pili katika michuano hiyo iliyoandaliwa na Shirika la Street Child United na kufanyika nchini Urusi

Tumi hiyo ya Tanzania mpaka inaingia hatua ya fainali ilikuwa haijapoteza mchezo hata mmoja na hivyo mchezo wa fainali waliofungwa ndio mchezo pekee waliopoteza. Mpaka inaingia hatua ya fainali ilikuwa imeshaweka rekodi ya kufungwa goli moja tu katika michuano hiyo

Katika hatua za makundi, Tanzania ilicheza na timu za Urusi, Kazakhstan. Ilicheza na Marekani katika hatua ya robo fainali na kisha lkuitoa England kwenye nusu fainali.

Itakumbukwa kuwa mwaka 2014 nchini Brazil, timu ya wavulana walio kwenye mazingira magumu ilichukua ubingwa kwa kuifunga Burundi.
 
Afadhali wakina dada wanajua wanachokifanya kuliko wale wauza sura wetu pamoja na kwamba wanalipwa hela nyingi lakn hakuna mafanikio.
 
Hivi na kocha wao ni wa mitaani? Mlivyoona mafanikio ya watoto wa mitaani mkachukua kocha majumbani?
 
wakimaliza wanarudi mtaani au? maana wakikaa majumbani si watakosa sifa za kushiriki kwa mara nyingine
 
Tanzania Girls wamefungwa goli 1 kwa 0 dhidi ya Brazil kwenye fainali ya kombe la dunia la watoto wa mtaani.Brazil ni mabingwa wapya sasa.
DSC6057-e1526477364929-992x561.jpg
 
Hongera kwao..b.t.w mchakato wa kuwapata ulikuaje? Maana mmh..
 
Jamani, inasikitisha sana. Kwahiyo wakirudi bongo wanarudi mtaani?!

Au hawa wasichana walikuwaga wa mtaani lakini sasa wako kwenye vituo? Naomba kueleweshwa.
 
Hongera sana sana!
Huwa wako wapi hawa watoto kwa ajili ya kuwapatia misaada?
 
Jamani, inasikitisha sana. Kwahiyo wakirudi bongo wanarudi mtaani?!

Au hawa wasichana walikuwaga wa mtaani lakini sasa wako kwenye vituo? Naomba kueleweshwa.
Me too walahi
 
Back
Top Bottom