Timu ya Tanzania ya Watoto waishio katika mazingira magumu yashika nafasi ya pili katika Kombe la Dunia

Timu ya Tanzania ya Watoto waishio katika mazingira magumu yashika nafasi ya pili katika Kombe la Dunia

Jamani, inasikitisha sana. Kwahiyo wakirudi bongo wanarudi mtaani?!

Au hawa wasichana walikuwaga wa mtaani lakini sasa wako kwenye vituo? Naomba kueleweshwa.
Kuna kituo konawalea kiko Mwanza, mwaka 2014 walienda wavulana walirudi na kikombe, mwaka huu ndio walipelekwa wadada
 
Wakirejea waende Dodoma bungeni kupongezwa. Sijui mafanikio haya yatawatoa mtaani?
 
Chanzo cha Habari BBC.
Timu ya taifa ya Tanzania kwa watoto wa mitaani imenyakua Kombe la Dunia kwa watoto wa mitaani, katika mashindano yaliyozishirikisha timu za mataifa mbalimbali duniani huko Rio de Janeiro, Brazil hapo jana.
Ikiwa imetinga fainali za Kombe la Dunia kwa watoto wa mitaani kwa mara ya pili mfululizo, timu hiyo ya Tanzania imeweza kutwaa Kombe la Dunia kwa Watoto wa Mitaani kama linavyojulikana Street Child World Cup hapa Rio de Janeiro.
Katika mechi ya fainali Tanzania iliibanjua Burundi iliyokuwa ikipewa nafasi kubwa ya kulinyakua kombe hili kwa Kuinyuka magoli 3-1 huku mchezaji kiungo mshambuliaji wa Tanzania Frank William akipiga magoli matatu na kuwa nyota wa mchezo. Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Tanzania ilikuwa ikiongoza kwa magoli 2-0. Kipindi cha pili iliongeza bao la tatu. Burundi iliweza kupata bao la kufutia machozi zikiwa zimebakia dakika nne mpira kumalizika.
Tanzania imetwaa ubingwa huo baada ya kuonyesha kiwango cha juu hata kuzishinda timu ngumu kama Burundi, Marekani, Indonesia, Nicarague, Ufilipino na Argentina.
Golikipa wa Tanzania Emmanuel ameweza kuchaguliwa kuwa golikipa bora wa michuano hii ya kombe la dunia.
Hii ilikuwa mara ya Pili kwa timu ya Tanzania kutinga fainali za michuano hiyo ya dunia kwa watoto wa mitaani inayofanyika siku chache kabla ya fainali za Kombe la Dunia kuanza mwezi Juni. Ikumbukwe kuwa fainali zilizopita za michuano hii kule Durban Afrika Kusini mwaka 2010 Tanzania ilifungwa na India katika fainali.
Mashindano haya hutambuliwa na Shirikisho la Soka Duniani, FIFA.

Source: Timu ya Watoto wa Mitaani wa Tanzania Watowa Kombe la Dunia Kwa Watoto wa Mitaani Mwaka 2018/2019. - ZanziNews
 
Hongera vijana, kwa hiyo huwa wakimaliza hiyo michezo wanarudi tena mitaani?
 
Hongera sana kwa hawa watt.

Sio hawa wengine wanalipwa mishahara mikubwa, offer kibao wanawafadhili lukuki lkn hata tu kushinda kombe ya kagame ni ishu. Yaan timu ya taifa, vpl timu zote wanatakiwa kuona haya sana kwa hili
 
yani maana yake tuna mitoto ya mitaani mingi sana kupita nchi zote duniani.

shenzi
 
Hongera zao, wametuwakilisha vizuri sana na kulitangaza Taifa. Sasa wasaidie kwa kila kitu.
 
Kwahyo nchi yetu ina watoto bora wa mtaani?
Ulaya hakuna watoto wa mtaani ndio maana tumewashinda
 
niliposkia taarifa zao nikapata matumaini angalau sasa bongo nayo inaenda kuwa na wawakilishi wa maana kwenye michuano ya kimataifa upande wa michezo
 
Let be realistic, hivi kweli hao ni watoto wa mtaani?
Nani anaweza kuthibitisha kuwa hao waliokwenda kushindana katika mashindano hayo kutoka nchi mbalimbali ni watoto wa mitaani?

Kwa uchunguzi wangu mdogo nimegundua karibu watoto wote waliokuwepo kwenye hicho kikosi cha Tanzania kilichoshiriki mashindano hayo ni watoto wanaotunzwa vizuri na kufundishwa kwenye kituo maalum cha michezo jijini Mwanza. Hao ni watoto wanaotunzwa vizuri kuliko watoto wa majumbani.

Ninawapa Hongera kwa ushindi huo.
 
Let be realistic, hivi kweli hao ni watoto wa mtaani?
Nani anaweza kuthibitisha kuwa hao waliokwenda kushindana katika mashindano hayo kutoka nchi mbalimbali ni watoto wa mitaani?

Kwa uchunguzi wangu mdogo nimegundua karibu watoto wote waliokuwepo kwenye hicho kikosi cha Tanzania kilichoshiriki mashindano hayo ni watoto wanaotunzwa vizuri na kufundishwa kwenye kituo maalum cha michezo jijini Mwanza. Hao ni watoto wanaotunzwa vizuri kuliko watoto wa majumbani.

Ninawapa Hongera kwa ushindi huo.
hata kama wanatunzwa vizuri lakini chanzo chao ni kutoka mitaani.
 
Back
Top Bottom