Timu ya utetezi ya Sean "Diddy" Combs yamaliza kesi bila kuita shahidi yeyote

Timu ya utetezi ya Sean "Diddy" Combs yamaliza kesi bila kuita shahidi yeyote

Manyanza

Platinum Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
22,269
Reaction score
58,563
Katika hatua ya kushangaza, upande wa utetezi katika kesi ya sex trafficking inayomkabili msanii maarufu Sean “Diddy” Combs umemaliza kutoa hoja zake bila kumuita shahidi yeyote mahakamani. Hii inamaanisha kuwa Diddy hatatoa ushahidi wake mwenyewe wala kuleta mtu yeyote kujitetea.

Upande wa mashtaka tayari ulikuwa umewasilisha ushahidi wake, ikiwa ni pamoja na ushuhuda kutoka kwa waliodai kuwa waathirika wa unyanyasaji wa kingono, na sasa jaji atatoa maelekezo ya mwisho kabla ya kuanza kwa majadiliano ya majaji.

Kumaliza kesi bila shahidi mara nyingi huwa ni mbinu ya kisheria inayotumika iwapo wakili wa utetezi anaamini upande wa mashtaka haujaweza kuthibitisha kesi yake "beyond reasonable doubt" (bila shaka yoyote ya msingi).

Kesi bado inaendelea
 
Back
Top Bottom