Timu ya yanga ikiwa mazoezini wanafanyaga nini msimu wa 2020/2021

Timu ya yanga ikiwa mazoezini wanafanyaga nini msimu wa 2020/2021

Kinachoiua yanga ni uongozi kukubali pressure iwafike kisha ikawafikia benchi ufundi na ikawaathiri wachezaji uwanjani...timu inaongoza ligi lakini ina pressure kubwa ya kutokubeba ubingwa ni maajabu....walipaswa kuwa na mbinu ya kulidhibiti hili unaikumbuka simba iliyokuwa inapigwa 5 mechi za klabu huku ikiwa nyuma ya yanga lakini Manara akawalinda wachezaji kwa kufanya pressure kubwa mtandaoni iwe kwake yeye na sio wachezaji, Uongozi wa juu nao ukawalinda wachezaji na kinyume chake ndicho kinachotokea yanga.
 
Wakuu Habari zenu?

Hivi hii timu ya yanga kwenye mazoezi wachezaji wanafanyaga nini? Au wanafanyaga mazoezi ya kukimbia tu? Maana wanavyocheza uwanjani ni kama watoto washule ya msingi ukiwaambia hapa chezeni mpira hapa.

Watajipanga kama yanga wanavyojipanga na watacheza kama yanga wanavyocheza yaani ukipata mpira wewe peleka mbele tu itajulikana mbele huko.

Inavyoonekana mwalimu hafundishi mpira hapo wala hakuna analysis zozote zinazofanyika kumuusu mpinzani wao wanaocheza naye, wao wanacheza tu kupeleka mpira mbele.

Sasa kama ndio hivyo kwenye mazoezi kocha anafundisha kwa kutoa maelekezo gani au ndio kocha anachukua mshahara wa bure yupo tu kama pambo .

Namna yanga wanavyocheza ni mpira ambao hauna maelekezo ya mwalimu iko wazi kabisa hiyo.

Soka la yanga limeshapitwa na wakati watu siku hizi wanacheza kwa utaratibu.

Kuna watu wanashangaa wavyopata ushindi wa goli na na sare,lakini ukifatiliA wavyocheza wao hawaweki mpira chini wao ni kurusha ndege tu. Kwa style hiyo kupata matokeo ni ngumu sana.

Msimu huu wataukosa ubingwa sijui watafanyaje maana msimu umeanza wamesajiri wachezaji kibao.na ubingwa wanaukosa .

Wachezaji wengi wa yanga wana miili mikubwa yaani kama mabondia sasa watu kama hao ukiwa nje ya box unawaambia pale au ndani ya box wamaambie lengeni tu goli maana kwa miili ile hakuna kipa wakudaka mshuti yao.ila wapi wao wanajichezea tu.
Hata mimi najiulizaga haya, kama jana KMC wangekuwa clinical, tungepigwa hata 5.
 
Back
Top Bottom