Timu za Premier League Zaweka Rekodi....

RRONDO

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2010
Posts
55,727
Reaction score
123,094
Timu za Premier League zimeweka rekodi mpya ya Timu Tano zote kuingia hatua za mtoano za Champions League. Chelsea,Liverpool,Manchester United,Manchester City na Tottenham Hotspur zote zimefuzu hatua ya 16 bora.

Msimu huu ni wa kwanza kwa timu tano za Premier League na hii ni baada ya Manchester United kufuzu kupitia Europa League, na zote tano zimeingia hatua za 16 bora. Hii ni mara ya kwanza tangu msimu wa 2013/14 timu zote za Premier League kupita hatua ya makundi, na hii inaonesha kuimarika kwa Premier League msimu huu.

Katika timu hizo tano ni Chelsea tu kamaliza nafasi ya pili, timu nyingine zote zimemaliza kama washindi kwenye makundi yao. Tusubiri tuone kama zote zitapita na kuingia robo fainali.

Premier League clubs set a new Champions League record

Seville vs Manchester United
Porto vs Liverpool
Basel vs Man City
Spurs vs Juventus
Chelsea vs Barcelona
 
Wakiiingia Robo Fainali hapo ndio itakuwa kipimo kizur sana kwa Team za Epl Kujua Ubora wao.
Ila so far Wamejitahid ila uwepo wa makocha hawa imesaidia sana kufanya lligi iwe na ushindan kwa maana wote hao wanaangalia mafanikio ya Champions League kama kipimo tosha cha mafanikio ya Team zao.
Man City - Guadiola
Man Utd - Jose Msema ovyo
Liverpool - Klopp
Chelsea - Konte
Totenham - Pochetino
 
Hapana, hicho ndio kipimo cha kwanza kuingia kwenye mtoano.
 
Nafikiri ilikuwa wapoteze nafasi moja kama wangeendelea kusuasua kama misimu michache nyuma.
 
Nafikiri ilikuwa wapoteze nafasi moja kama wangeendelea kusuasua kama misimu michache nyuma.
Nafas yao ilikuwa ichukuliwe na Team za Italy nafikr ile mwaka jana kuna kiwngo cha points ambazo team za italy walitakiwa kufikisha ambazo hawakufanikiwa
 
Uefa wanaanza kuhesabu hapo. Kwahiyo mwakani itaongezeke nafasi moja.
Hamna nafasi itakayoongezeka. England,Spain na Germany wanapewa nafasi NNE tu, huku Italy,Portugal na France wanapewa nafasi tatu kwa mujibu wa Euro coefficient(perfomance). England wamepata tano kwasababu MAn Utd kashinda Europa League na kamaliza nje ya top 4.
 
Mbona unajipinga mwenyewe? Au hujui, tulia nitakuelewesha.
 
Mbona unajipinga mwenyewe? Au hujui, tulia nitakuelewesha.
 
Mbona unajipinga mwenyewe? Au hujui, tulia nitakuelewesha.
Ingekuwa UK wanatakiwa wawe na nafasi 4 tu, kama ulivyosema. Basi mshindi wa 4 angeondelewa ili Man U achukue nafasi yake. Kama ameenda na Man U wameenda ujue hujui taratibu zake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…