Timu zenu zikiwapata hawa wachezaji zitakuwa zimelamba dili

Timu zenu zikiwapata hawa wachezaji zitakuwa zimelamba dili

Smart AJ

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2022
Posts
5,564
Reaction score
5,884
Ni wachezaji wa ndani kabisa, ila wanajua sana soka, wanacheza namba mbalimbali.

Wako wengi ila jicho langu limewaona wafuatao, na nina imani kwa mtu mwenye jicho la mpira basi hatasita kukubalinana nami hata kidogo.

[emoji599]Kelvin Kijiri - Beki wa kulia (KMC)

[emoji599]Hance Masoud Msonga - beki wa kushoto (KMC)

[emoji599]Hassan Nassoro Mulid - Kiungo mkabaji (Mbeya City)

[emoji599]Yahya Mbegu - Beki wa kushoto (Geita)

[emoji599]Sixtus Sabilo - Kiungo mchezeshaji (Mbeya City)

[emoji599]Greyson Gwalala - Kiungo mchezeshaji (Coastal Union)

[emoji599]Baraka Gamba Majogolo - Kiungo mkabaji (KMC)

[emoji599]Kelvin Nashon - Kiungo mkabaji (Geita)

[emoji599]Adam Adam - Mshambuliaji (Mtibwa)

[emoji599]Roland Msonjo - Beki wa kati (Ruvu Shooting)

[emoji599]George William Makang'a - Winga (KMC)

[emoji599]Joseph Mahundi - Kiungo

[emoji599]Mbaraka Yusuph - Kiungo (Kagera Sugar)

[emoji599]Clement Mzinze - Mshambuliaji (Yanga)

[emoji599]Frank Charles Magingi - Beki wa kati (Namungo)

Na wengine wengi wazuri, hongera kwao.[emoji1487]
 
Naongezea wakwangu

Issa abuushee kijana anajua ball na guu lake lake la kishoto anacheza winga coastal union

Tepsi evance ,nataman awe ana cheza kila mechi mana ananikumbusha enzi zangu Azam fc

Kadikilo anacheza geita gold jamaa anajua sana ila watanzania wanamkaushia

Hamadi maji mengi a.k.a hotwater jamaa anacheza vizur sijui kwann kibu yupo simba alafu maji mengi yupo coastal.
 
Nimejiuliza sana na naona watu wengi wanajiuliza sana kuhusu wachezaji wengi wa kibongo wakiwa timu ndogo wanawika sana lakini wapeleke timu kubwa Simba na Yanga ambazo hushiriki michezo ya kimataifa mara kwa mara ghafla wanapotea kabisa. Miaka michache iliyopita Simba, Yanga na Cosatal kila moja ilikuwa na "Mesi" wake na wote walikuwa wanauwasha kweli kweli kiasi nikawa nasema baada ya miaka mitano ijayo hao wakina "Messi" wa kibongo watakuwa wanacheza Ulaya maana wakati ule walikuwa vijana sana. Kumbe nilikuwa naota tu, kwani sasa hivi hata kwenye ligi yetu ya NBC siwasikii kabisa.

Na huyo Tepsi akomae tu na Azam yake ikitokea timu nje inamuhitaji ndio aende zake. Akijichanganya tu na hawa Kurwa na Doto wa Kariakoo basi na yeye atabaki historia kama wenzake wakina "Messi" wa kibongo.
 
Huyu Mbaraka Yusuph si alienda azam, akachemka vibaya
 
Back
Top Bottom