Timu zenye nafasi ya kuwa bingwa wa EPL msimu ujao

manonawire

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2017
Posts
943
Reaction score
1,223
Habari wana jukwaa
Niende moja kwa moja kwny uzi

Katika mda huu ambao macho na masikio ya wapenzi wa soka yameelekea pale RUSSIA hebu turudi kidogo kwny ligi zetu pendwa za soka hasa ligi kuu ya ENGLAND
Mimi kwa mtazamo wangu kwny epl kuna timu tatu zina nafas kubwa ya kuwa bingwa msimu ujao

LIVERPOOL
Hawa jamaa inaonekana wamedhamiria kumaliza ukata wao wa mda mrefu wa kupata kombe lile pendwa la barclays hili wanalidhiirisha hata kwa aina ya usajili wanaofanya

CHELSEA
Hawa nawapa nafasi kwa sababu wana timu nzuri na bado kuna uwezekano wakarudisha majembe yao waliyoyatoa kwa mkopo hivyo kuwa fanya wawe na timu nzuri zaidi na ya ushindani zaidi

MAN UNITED
Mashetani wekundu wamedhamiria kweli kweli na msimu ujao wataongeza nguvu zaidi ili wawe mabingwa usajili wanaofanya unatosha kujieleza na wakiongezea mbinu za "the special one"

Toa na ww maoni yako kama mdau wa ligi ya EPL
 
kombe wakilikosa man city basi lipo united
 
Ngoma inaenda darajani ..hao watoto city mda wao tayari
 
time will tell ila kuna mdau mwaka jana alitabiri mpangilio wa timu na ukawa vilevile
 
Naona umeandika kama unaota, ngoja kwanza timu zisajili ziende pre season, nyingine zipate makocha and then ndo tuanze utabiri kutokana na hali za vikosi vyao, vinginevyo utakuwa unafanya ramli tu.
 
Naona umeandika kama unaota, ngoja kwanza timu zisajili ziende pre season, nyingine zipate makocha and then ndo tuanze utabiri kutokana na hali za vikosi vyao, vinginevyo utakuwa unafanya ramli tu.
Hakuna kaka timu kama arsenal kwa mwakan haiwez kubeba kombe
Naona umeandika kama unaota, ngoja kwanza timu zisajili ziende pre season, nyingine zipate makocha and then ndo tuanze utabiri kutokana na hali za vikosi vyao, vinginevyo utakuwa unafanya ramli tu.

Hata zisajili na ziende pre na pre season hao ndio wenye nafasi msimu ujao,broo au tungoje muujiza kama ule wa LEICESTER CITY
 
Mkuu liver watoe hawawezi tena kurudia mafanikio ya msimu huu,tayari pumzi ishawakatia,

Tottenham iwapo Pochettino ataendelea kuwepo wanaweza ishangaza dunia,Chelsea na Man city kati ya hizo 3 mmoja lazima awe bingwa
 
Hakuna kaka timu kama arsenal kwa mwakan haiwez kubeba kombe

Hata zisajili na ziende pre na pre season hao ndio wenye nafasi msimu ujao,broo au tungoje muujiza kama ule wa LEICESTER CITY
Kwahiyo kwa uwezo wako wa uchambuzi wa soka kwako wewe Man City hana timu ya kugombea ubingwa msimu ujao..?
Ahahaaaaaaah..!
Kwamba Liverpool na Chelsea wana timu bora kuliko Man City..?
Ahahaaaaaaah..!
Unamuweka Man Utd kwenye mbio za ubingwa wakati huo huo unamtoa Man City..?
Ahahaaaaaaah..!
Sio bure,kuna tatizo hapa..!
 
Mchuano utakua kati ya liverpool vs man city...
 
kweli wewe ni full of faith

Hata mimi nadhani itakuwa Arsenal, sijui kwanini..ila naogopa watakuwa wao...timu yangu ni Liverpool..lakini Arsenal nina wasiwasi nao..wamechekwa mno mwaka jana au msimuuliopita...wachezaji wao hawajahama, halafu wataongeza wachezaji wawili au watatu nyuma na kiungofoward yao nzuri tu ..nawaogopa hawa jamaa..watakuwa motivated na matokeo mabaya ya msimu uliopita
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…